Pelekeni watoto shule kwani Serikali imeshajenga vyumba vya madarasa ya kutosha.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akikabidhiwa vyumba vya madarasa 7 katika Wilaya ya Longido.
Amesema haina maana kama vyumba vya Madarasa vimekamilika alafu hakuna watoto wakusoma, walimu wakufundisha ni kazi bure.
"Acheni kuwapeleka watoto kuchunga mifugo, wapelekeni shule wakapate elimu yakuwasaidia baadae".
Umuhimu wa elimu kwa watoto itasaidia Jamii zenu kwani wataalamu mbalimbali watapatikana wakiwemo wataalamu wa mifugo, madaktari na wengine ili wake wafanye kazi katika Jamii hii.
Mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Nurdin Babu amesema kwa Wilaya yake ujenzi wa vyumba vya madarasa yaliyobaki yatakamilika ifikapo Disemba 20,2021.
Amesema Halmashauri hiyo ilipatiwa kiasi cha fedha Bilioni 2.6 kwa ajili ujenzi wa vyumba vya madarasa 64 yakiwemo ya shule shikizi 50 na Sekondari 14.
Mhe.Mongella ameanza ziara katika Halmashauri za Mkoa wa Arusha kwa lengo la kukabidhiwa vyumba vya madarasa vilivyokamilika ili kuwawezesha watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2022 wanaanza masomo ifikapo Januari 2022 mapema.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa