• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WATALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAMETAKIWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO

Posted on: December 17th, 2024

Na Elinipa Lupembe  



Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande amewataka washiriki kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yao huku akiweka wazi kuwa, Wizara ya Fedha  inaendelea kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wataalam wa Ununuzi na Ugavi.



Mhe Chande amesema hayo muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb) Doto Biteko  kufungua Kongamano la Watalamu wa Ununuzi na Ugavi, linalofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha, ukumbi wa Simba, leo Desemba 17,2024.



Mhe. Chande, amesema kuwa,  miongoni mwa mambo yanayosababisha mkwamo Serikalini ni pamoja na wivu, choyo na fitna miongoni mwa watumishi, hivyo amewataka kuondokana na mambo hayo ili kukua na kujiletea maendeleo.



"Tumieni Taaluma yenu kufanya kazi kwa weledi na  kuzingatia kanuni sheria na taratibu za taaluma na utumishi wa Umma, msiogope kulaumia kwa kuzingatia sheria na taratibu za kazi na hakikisheni mnakuwa waadilifu, waaminifu na kuachana na tabia za wivu, choyo na husda tabia ambazo zinazua migongano kazini zenye chuki, jifunzeni kuwa wastahimilivu na kusamehe zaidi" Amesema 



Amewasisitiza kutumia Taaluma zao kwa kuwa, Sheria ya Ununuzi wa Umma sura 410 inawalinda wataalam wa Ununuzi na Ugavi na kuwataka kutembea kifua mbele na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo.



Awali, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Benezeth Ruta ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha zinazoiwezesha taaluma hiyo kusonga mbele.



Amesema Bodi hiyo inaendelea na utekelezaji wa Sheria Na. 23 ya mwaka 2007 kuhakikisha kuhakikisha Wataalam wanaofanya shughuli za ununuzi na ugavi wana sifa stahiki za kufanya kazi hizo.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa