• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WATOTO 200 WAPATIWA KADI ZA BIMA YA AFYA

Posted on: March 7th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewakemia  vikali wazazi wote ambao watoto wao wanapata Mimba  wakiwa mashuleni kisha familia mbili zinakaa kusuluhisha kindugu kuacha mara moja tabia hiyo, badala yake kutoa taarifa sehemu husika ili hatua kali za kisheria zichuliwe.

Ameyasema hayo alipokuwa akiwakabidhi  kadi za bima ya afya kwa watoto 200 wanaotoka katika mazingira magumu na wengine yatima kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Amesema kwa kusuluhisha kindugu kunasababisha ongezeko la Mimba za utoto na kukatisha masomo na ndoto za watoto wengi wa kike.

Serikali inaendelea kukemia na kupiga vita mimba za utoto na kwamwe hatutafumbia macho wale wote watakaobainika kuwapa mimba watoto wa shule.

Aidha,Gambo amewataka wamiliki wa vituo vya makao ya watoto kufuata sharia zote za nchi na kuacha kuvitumia vituo hivyo kama njia ya kujipatia fedha na huku kiasi kidogo sana kikienda kwa watoto hao.

Pia, amewataka wamiliki hao kuzingatia maadili ya jamii yetu katika kuwalea watoto hao ili wakuwe kwenye mazingira ya maadili na tabia njema katika jamii yetu.

Ameipongeza benki ya Stanbic kwa kuona umuhimu wa kutoa bima hizo za afya kwa watoto 200 kwani wamewasaidia sana watoto hao hasa kwa kujali afya zao na amewataka wadau wengine kuiga mfano huo wa Stanbic benki, ili kulinda afya za watoto hao.

Mkuu wa Kitengo cha biashara Afrika kutoka benki ya Stanbic bwana Brayan Zwanzigira, amesema benki yao ipo pamoja kwa kushirikiana na serikali katika mambo mbalimbali ya maendeleo.

Amesema huduma hiyo watajitaidi kuendelea nayo kwa miaka kadhaa kadri watakavyoweza.

Nae Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha bwana Hargeney Chitukulo, amesema bado Mkoa wa Arusha una idadi ya watoto 54,000 wanaoishi kwenye mazingira magumu na kwa takwimu za kitaifa kwa mwaka 2017 hadi 2018 watoto 864,496 walibainika  wanaishi kwenye mazingira magumu.

Amesema bado kuna changamoto kubwa ya ukatili wa kijinsia kwa watoto hasa katika mimba na ndoa za utoto katika jamii yetu.

Benki ya Stanbic imetoa kadi za bima ya afya inayojulikana kama toto afya kadi iliyoanzishwa na mfuko wa bima ya afya kwa lengo la kuwasaidia watoto kupata huduma za afya kwa bei ya shilingi 50,400 kwa mwaka.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa