Watoto wenye mahitaji maalumu(ulemavu wa akili) 34 watunukiwa medali 32 baada yakuibika washindi katika mashindano ya Olimpiki MaalumuTanzania ali maalufu kama (SOT) yaliyofanyika mapema Zanzibar.
Akiwatunuku medali hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Emmanuel Maundo amesema nijambo lakujivunia sana kwa mkoa wetu kuibuka washindi katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na riadha,na kuweza kupata wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.
“Ninafuraha sana kuona watoto wetu wenye ulemavu wa akili wameweza kuuwakilisha vizuri mkoa wetu katika mashindano haya, na wameweza kuonyesha kuwa hata wao wanaweza kufanya vizuri sana katika michezo mbalimbali.”alisema
Amewasihi sana wazazi ambao bado wanaendela kuwaficha watoto kama hao waache mara moja kwani hata wao bado wana fursa kubwa katika jamii yetu,hivyo wanatakiwa kupewa nafasi kama ilivyo kwa watoto wengine.
Aidha, amezitaka halmashauri zote za mkoa wa Arusha kuhakikisha zinatenga bajeti maalumu yakuendesha michezo kwa watoto wenye ulemavu kama ilivyo kwa watoto wengine na kuhakikisha zinashiriki katika mashindao yajayo.
Serikali inatambua vizuri sana mahitaji ya kundi hili la watoto wenye mahitaji maalumu ndio maana ikatenga bajeti yakutosha mashuleni ili waweze kupata chakula chakutosha asubuhi na mchana.
Akiongezea zaidi,amesema ofisi ya mkuu wa Mkoa Arusha itaendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo nakutoa ushirikiano kila mara ili kuwasaidia watoto hao waweze kuendelea na michezo yao.
Pia mratibu wa SOT Bwana Antony Mushi, amesema timu ya watoto hao walemavu wa akili imeweza kuibuka na medali 6 za Dhahabu,12 za Fedha na 14 za Shaba nakufanikiwa kutoa watoto watatu ambao watashiriki mashindano yakimataifa yatakayofanyika Machi 2019,huko Abu Dhabi Uarabuni.
Amewashukuru wafadhili mbalimbali waliojitokeza katika kusaidia mahitaji mbalimbali ya timu hiyo hususani tiketi za mabasi kwenda Zanzabar na kurudi,vyakula na vifaa vya michezo.Amehimiza wasichoke kusaidia kwani bado uhitaji nimkubwa na kuomba na wafadhili wengine wajitokeze zaidi.
Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Onoka, nae amesema kama mkoa atahakikisha mashindao hayo ya watoto wenye ulemevu wa akili yanafanyika kila mwaka kwa Mkoa wa Arusha.
Amesema michezo kwa watoto hao nimuhimu sana kwa afya zao hivyo hamna budi kuyafanya kila mwaka badala yakusubiri kila baada ya miaka 3 au 4.
Olimpiki maalumu kwa Mkoa wa Arusha ilianza mwaka 1990 kwa mashindano hayo kufanyika hapa hapa Arusha na baadae yaliendelea katika mikoa mingine nchini.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa