Na Elinipa Lupembe
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (Mb) amekutana na kufanya kikao na kamati ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi wakiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Chtistian Makonda pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Aprili 20, 2024.
Katika kikao hicho Mhe. Katambi amewaponheza wajume wa kamati hiuo ya maandalia kupitia Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha iongozwa na Mkuu wa mko na Katibu Tawala wa mkoa huo, kwa kazi nzuri na mipango mizuri iliyofanyika mpaka sasa, jambo ambalo linatia moyo kuwa Mei Mosi 2024 itakuwa ya tofauti.
"Nimefarijika sana kwa kazi nzuri na kubwa ya maandamizi iliyofanyika mpaka sasa, inaonesha ni jinsi gani wanakamati wanajituma licha ya majukumu mengi ya kikazi waliyo nayo, endeleeni na moyo huo mpaka Siki yenyewe ya Mei Mosi, tukampambe Mhe Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan" Amese
Amewata wajumbe wa kamati ya maandalizi kuendelea kushirikianaa kwa karibu ili kukamilisha shughuli walizopangiwa kwa wakati na hatimaya kufikia malengo ya Siku maalum ya Wafanyakazi Duniani ambao ndio wajenzi wa Taifa la Tanzania.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kila Kamati inafanya kazi kikamilifu na kuhakikisha kuwa sherehe hizo zinafana.
Aidha, Mhe. Makonda amewasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo, ambayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika kikao hicho pia wameshiriki Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakioongozwa na rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Arusha, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Missaile Musa, Makamishna wa Kazi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zake.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa