• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MCHENGERWA AAHIDI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MUNDARARA

Posted on: September 18th, 2024


Na Elinipa Lupembe 



Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa @mohamed_mchengerwa ameahidi  Serikali kutoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Mundarara wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.



Mhe. Mchengerwa ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Mundarara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mundarara Septemba 18, 2024, kufuatia ombi la wananchi hao kutokana na uhitaji mkubwa  wa huduma kituo cha afya katika eneo lao, unaotokana na idadi kubwa ya watu wanajishughulisha na uchimbaji wa madini.



Amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufikishia kwa wananchi huduma zote muhimu ikiwemo huduma za afya, elimu, miundombinu ya umeme, barabara na maji na kusisitiza kuwa Serikali itatoa fedha na ujenzi utaanza mara moja.



"Niwaahidi wananchi wa Mundarara, Serikali itatoa shilingi milioni 300 na Kituo cha afya kitajengwa hapa Mundarara, Rais wetu anayo nia dhati ya kuhakikisha kila mtanzania anafaidi matunda ya nchi yake, huduma zote za msingi ni haki ya kila mtanzania". Amesema



Hata hivyo ameahidi kutoa milioni 125 kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Longido - Mundarara na daraja la Matiani na kuuiagiza Uongozi wa TARURA mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na TARURA wilaya ya Longido kuanza mara moja ujenzi wa daraja hilo, linalounganisha kata hiyo ya Mundarara na kata nyingine, daraja ambalo lilibomoka wakati wa msimu wa mvua za mwaka huu na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.



"Ninawaagiza TARURA anzeni mara moja ujenzi wa  daraja hilo ili wananchi wapate huduma ya usafiri kwa haraka , eneo hili ni muhimu sana kutokana na shughuli za uzalishaji wa madini pamoja na muingiliano mkubwa wa kibiashara, hivyo wananchi hawatakiwi kukwama kutokana na miundombinu ya barabara, tengenezeni daraja ili huduma hiyo irejee kama awali". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa



Mhe. Mchengerwa yuko mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi mkoani humo.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa