" Nakuagiza Waziri wa Maji ndani ya miezi 3 yani kufikia mwezi Machi 2023 mradi wa bilioni 1.7 wa hapa Monduli uanze kufanya kazi".
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza na wananchi wa Makuyuni Wilayani Monduli.
Amesema, serikali itaendelea kutafuta fedha zakuwezesha miradi mingine ya Maji wilayani humo kukamilika ikiwemo mradi wa Maji wa Jiji la Arusha ambao unauwezo wakupeleka Maji Monduli.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema wilaya hiyo imepokea fedha zaidi ya bilioni 1.6 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amemshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi za miradi ikiwemo ya Maji katika Mkoa wa Arusha.
Rais Samia, amewasili Mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi akitoka Mkoa wa Manyara na kupokelewa eneo la Makuyuni Wilayani Monduli.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa