Na Elinipa Lupembe
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Visiwani Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi anatarajiwa kuzindua mradi wa kwanza wa uwekezaji katika visiwa vidogo vilivyoko Kisiwa cha Bawe tarehe 15 Juni mwaka huu 2024.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 07, 2024 na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Visiwani Zanzibar Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa onesho la Karibu Kili Fair 2024, akiwakaribisha washiriki wa onesho hilo kuhudhuria uzinduzi huo ikiwa ni mpango maalum wa kuvihuisha visiwa vidogo vinavyopatikana kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.
Mwaka 2021 serikali ya Zanzibar iliruhusu uwekezaji kwenye visiwa vidogo vilivyopo Unguja na Pemba ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali ya kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya utalii na uchumi wa buluu ili kuongeza pato la Taifa.
Katika hatua nyingine, Waziri Soraga amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Chrisrian Makonda kwa kutambulisha na kumuomba Rais Mwinyi kusaidia katika kuiunganisha Zanzibar na Arusha kiutalii, akisema mpango huo utasaidia katika kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo ya Utalii yenye kuingiza fedha nyingi za kigeni.
Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yamezinduliwa leo Mjini Arusha na Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Angellah Kairuki aliyeambatana na Waziri wa utalii Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Hassan Abbas na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda na wageni wengine kutoka ndani na nje ya TanTanzan
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa