NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa, Dk. Grace Magembe ametoa amewataka Waandishi wa habari za mitandaoni kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao katika kuripoti uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 ,2024.
Dk.Magembe ametoa maelekezo hayo Novemba 13,2024 wakati akifungua semina ya Waandishi wa habari za mitandaoni iliyoandaliwa na TAMISEMI ikiwa lengo ni kuwaelimisha kuhusu kanuni za uchaguzi wa serikali za Mitaa,2024.
Amesema Waandishi wa habari wanapaswa kutoa taarifa sahihi kwa wananchi hivyo ni vyema kujengewa uwezo kwenye Kanuni ili waweze kuwa na uelewa mpana wa kanuni na kuhabarisha wananchi ili wajue umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi pamoja na kupima sera na maono ya wagombea wa nafasi hizo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa eneo husika.
“Naomba niwasisitize mambo kadhaa ikiwemo kuandika habari zinazosimamia misingi ya haki na usawa kwa wagombea wote ili kuleta utulivu na amani nchini” amesema Dk.Magembe.
Ameongeza kuwa,”Epukeni kuripoti habari za taharuki kwenye nchi,msisababishe uvunjifu wa amani,epukeni taarifa za kuwatenganisha Watanzania bali mripoti habari zenye kuleta mshikamano na upendo katika kipindi hiki cha uchaguzi” amesisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa TAMISEMI
Pia amewataka Wasamizi wa Uchaguzi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kuweka mazingira bora ya ufanyaji kazi kwa waandishi wa habari wakati wa Uchaguzi!
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa