Wilaya Ngorongoro ni mojawapo ya Wilaya sita zilizopo katika Mkoa wa Arusha.Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1982 chini ya sharia namba 5 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. “The Local Government Instrument 1982”. Sehemu kubwa ya Halmashauri hii ni eneo la Serengeti Ecosystem.
Ukubwa wa eneo la Wilaya ni kilometa za mraba 14,036 ambalo lipo katika nyuzi 30030’ kusini mwa Ikweta na 35042’ Mashariki mwa Greenwich na urefu wa mita 1,009 hadi 3,645 kutoka usawa wa bahari. Ngorongoro inapakana na Nchi jirani ya Kenya kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Serengeti kwa upande wa Magharibi, Wilaya za Monduli na Longido kwa upande wa Mashariki na Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini.
Hali ya hewa
Kwa ujumla Wilaya ya Ngorongoro ina maeneo ya joto la washastani hasa katika Tarafa ya Sale na hali ya Kitropikali Wilaya Ngorongoro ina mvua za wastani wa 800mm hadi 1,000mm na upepo Mkali unaovuma kutoka Mashariki kuelekea Magharibi. Maeneo makubwa ya Wilaya ya uoto wa asili jamii ya Akashia hasa ukana wa Kati, Mashariki na Magharibi. Upande wa Mashariki na Magharibi kuna Ukanda wa bonde la Ufa na misitu Mkubwa. Upande wa Kusini mwa Wilaya ni eneo maarufu la Hifadhi ya Ngorongoro linalochukua asilimia 59 ya wilaya ambalo lipo katika Tarafa moja ya Ngorongoro. Eneo hili lipo chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa