MAJUKUMU YA KITENGO CHA TEHAMA
Kuratibu uundwaji wa Mpango Mkakati wa TEHAMA, sera, miongozo na waraka unaoendana sanjari na sera ya TEHAMA ya taifa.
Kuratibu utekelezaji wa mifumo ya menejimenti ya taarifa kwa Wizara, Idara, Wakala na wadau wa mkoa.
Kutengeneza na Kuhuisha Tovuti ya Mkoa na Halmashauri zinafanya kazi kwa ufanisi.
Kusimamia, kufuatilia na kutoa msaada wa kiufundi katika Mifumo yote iliyosimikwa katika sekretarieti ya mkoa na mamlaka ya serikali za mitaa.
MIFUMO ILIYOPO MKOA WA ARUSHA
Mfumo Funganishi wa Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha
(IFMIS-Epicor 9.05).
Mfumo wa Ukusanyaji Mapato (kodi na tozo) – LGRCIS
Mfumo wa malipo kwa kutumia mashine za Kieletroniki - MAXCOM
Mfumo wa kutunza kumbukumbu za mali za Halmashauri - ( System for Operation,Maintainance and management of Assets(SOMMA))
Mfumo wa Malipo “Tanzania Interbank Settlement System” - TISS
Mfumo wa Kutunza Kumbukumbu wa Watumishi (HCMIS – LAWSON)
Mfumo wa takwimu za Elimu msingi – BEMIS na PREM
Mfumo wa kumbukumbu na takwimu za Kazi TASAF – PWP
Mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Vituo vya Kutolea huduma za Afya – GoT HoMIS
Mfumo wa kuandaa mipango na Bajeti na kutoa ripoti – (SBAS and PlanRep)
Mfumo wa kukusanya na kuhifadhi takwimu – LGMD
Mfumo wa kusimamia Afua za UKIMWI – TOMSHA-TACAIDS.
Mfumo wa Kodi Ardhi – LRMIS
Mfumo wa kijiographia – GIS
Mfumo wa kusimamia mahudhurio – (Biometric Time and Attendance Monitoring System).
Mfumo wa barua pepe za serikali - GMS
Tovuti ya Mkoa na Halmashauri – GWF
Kusimamia, kufuatilia na kutoa msaada wa kiufundi katika miundombinu ya mawasiliano iliyopo katika sekretarieti ya mkoa na Mamlaka ya Serikali za Mataa, miundombinu hiyo ni pamoja na
Miundombinu ya OR – TAMISEMI, IFMIS – EPICOR – VSAT/RADIO/FIBER
Miundombinu ya mawasiliano ya mtandao wa internet
Miundombinu ya mawasiliano ya simu/nukushi – TTCL.
HALI YA MIFUMO YA KISERIKALI
Kitengo cha TEHAMA kimekuwa kikisimamia mifumo mbalimbali ya kiserikali ikiwepo Mfumo wa Kukusanya Mapato(LGRCIS),Mfumo huu umeunganishwa katika mfumo wa fedha(EPICOR) na unatumika katika kukusanya mapato yote ya vyanzo vya ndani.
Wataalamu wa Mkoa(Afisa TEHAMA na Afisa Msimamizi wa Fedha) wamesimika Mfumo huu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa maana ya Halmashauri za Mkoa wa Arusha. Kwa maeneo yaliyo nje ya makao makuu ya Wilaya/halmashauri vifaa maalumu aina ya ‘POS’ hutumika. Jedwali lifuatalo inaonyesha mchanganuo na tathimini ya Vifaa hivi kwa kila Halmashauri.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa