MAJUKUMU
1.To asssist,coordinate backstopping and monitor operation and maintenance for water supply schemes in LGA's.
2. To facilitate LGA's in developing guidelines for operation and maintenance of water supply schemes in the repsective community projects and private operated schemes.
3.To facilitate provision of technical expertise to LGA's to suppport communities,institutions and private sector in operation and maintenance of water supply schemes.
4.Monitor and supervison of implementation of projects.
5.To coordinate, review and give recommendations on designs submitted by LGA's for water supply projects infrastructures.
6.To ccordinate and harmonize approaches for water sector implementation and standards of engineering for Urban and Rural water supply.
7. Representation of the Ministry of water in interpreting the National Water Sector Policies andf guidelines for Urban and Rural Water Supply.
8. Facilitating,coordinating and advice LGA's in implementation of NRWSSP activities including appraisal of Districts projects,Procurement of services from Contractors and Consultants and application of Public Procurement Act and Regulations, Budgeting and Financial Management.
9. To facilitate provision of linkage between LGA's ,other relevant authorities and the MoW in the planning and development of water sector components.
10. To facilitate provision of technical expertise and advice to LGA's in capacity building and support for community owned water supply organisation (COWSOs) in operation and maintenance of water supply schemes.
11. Helping LGA's in preparing the guidelines for implementation and rehabilitation of water projects i.e Design of water projects,preparation of Bill of Quantities (BOQ),preparation of Tender documents,Evaluation of bids,preparation of contracts documents,supervision and coordination of Construction of water schemes, setting out and surveying,attending different Regional Meetings, Planning and Budgeting.
Hali ya huduma ya Maji
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi waishio vijijini katika Mkoa wa Arusha imeendelea kuimarika siku kwa siku, mpaka sasa asilimia 70.2 ya wakazi waishio vijijini katika Mkoa wa Arusha wanapata huduma ya maji safi na salama kupitia miradi ya maji inayotoa huduma iliyopo. Aidha, jumla ya vijiji 304 kati ya 390 vinahuduma ya maji rasmi na vijiji 86 havina huduma rasmi ya maji. Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini imepanga kuvipatia huduma ya maji vijiji vyote visivyo na huduma rasmi ya maji ifikapo 2024, katika Mkoa wa Arusha.
Serikali kupitia RUWASA Mkoa wa Arusha katika kipindi cha bajeti 2021/2022 imeendelea kujenga miradi mipya,kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji maji vijijini, ambapo jumla ya miradi 66 yenye thamani Tsh.32,610,648,952.64 inaendelea kutekelezwa na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji, Aidha, miradi hii ikikamilika itapunguza idadi ya vijiji visivyo na huduma ya maji rasmi kutoka 86 hadi 63, na hivyo kuboresha hali ya huduma ya maji vijijini kwa kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 70.2 ya sasa hadi asilimia 76.2, ifikapo Juni, 2022.
Katika bajeti ya 2021/2022 RUWASA Mkoa wa Arusha iliidhinishiwa jumla ya Tsh.10,276,348,023 Kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini, hadi sasa jumla ya Tsh.4,396,637,286.90 zimepokelewa sawa na asilimia 42.9 ya bajeti. Aidha, tulipokea bajeti ya ziada kiasi cha jumla ya Tsh. 2,470,881,598.03 kupitia program ya mpango wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji 5 vijijini ambapo hadi sasa utekelezaji unaendelea katika hatua mbalimbali.
Katika usimamiaji wa huduma ya maji kwa skimu za maji zilizokamilika, Mkoa wa Arusha kupitia RUWASA imeendelea na zoezi la uhuishaji na uundaji wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii kama inavyoelekezwa na sheria ya huduma za maji Na.5 ya mwaka 2019, ili kuimarisha huduma ya maji vijijini na kuwa na uendelevu wa miradi ya maji. Hadi sasa jumla ya vyombo 97 kati ya 101 vimehuishwa na kusajiliwa kisheria kwa ajili ya kusimamia utoaji wa huduma ya maji ngazi ya jamii.
Hali ya Huduma ya Maji Mjini
Kuhusu utaoji wa huduma ya maji mijini, Serikali Mkoani Arusha inatekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya kimkakati yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji mijini kwa kiwango cha asilimia 100. Hivi sasa, miradi hiyo inaendelea kutekelezwa katika meneo mbalimbali kama ifuatavyo:
Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Arusha kwa gharama ya Shilingi Bilioni 520 utakapokamilika. Mradi huu pamoja na shughuli nyingine unahusisha uchimbaji wa visima virefu 56 na unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwa zaidi ya asilimia 100 ikiwa ni pamoja na:
Kuongeza kiwango cha kuzalisha maji kutoka wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.
Kuongeza idadi ya wakazi wanaopata maji kutoka wastani wa 325,000 hadi kufikia 600,000 wakiwemo wastani wa watu 250,000 wanaoingia na kutoka Jijini kila siku.
Kupunguza upotevu wa maji kutoka wastani wa asilimia 40 hadi asilimia 25.
Kuongeza mtandao wa maji safi kutoka asilimia 44 ya sasa hadi asilimia 100;
Kuongeza mtandao wa kukusanya majitaka kutoka asilimia 7.66 hadi asilimia 30
Mpaka sasa, hali halisi ya utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 70 na umepangwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2022. Mamlaka imeweza kuongeza huduma ya upatikanaji majisafi na huduma ya uondoaji majitaka imeimarika katika Jiji la Arusha. Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio na faida zilizopatikana baada ya utekelezaji wa mradi kuendelea: -
Mahitaji ya maji katika Miji midogo Mkoa wa Arusha
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji mdogo wa Longido lita 1,501,000, Mji mdogo wa Ngaramtoni lita 7,444,240, Mji mdogo wa Monduli lita 2,038,890 na Mji mdogo wa USA River lita 4,114,500) wakati maji yanayozalishwa ni lita 70,000,000 kwa siku sawa na asilimia 63.8% ya mahitaji kwa siku.
Matarajio ni kufikia asilimia 100 ifikapo mwezi Juni, 2025 baada ya kukamilika kwa miradi inayoendelea kutekelezwa. Mamlaka imepanga kuongeza mtandao wa majisafi kwa zaidi ya kilomita 453.829 katika maeneo mbalimbali (lengo ni kuongeza kilomita 200 jiji la Arusha, kilomita 30.561 mji wa Ngaramtoni, kilomita 95 mji wa Monduli, kilomita 73.268 mji wa USA River na kilomita 55 mji wa Longido). Ongezeko hili la mtandao litapelekea huduma ya majisafi kuongezeka kutoka asilimia 72.3 ya sasa na kufika asilimia 100. Aidha, Mamlaka imepanga kufanya maunganisho mapya kwa wateja 41,978 hadi kufikia mwaka 2025/26, ambapo utekelezaji wa mpango huo umeanza.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa