Sekta ya elimu katika mkoa wetu inaendelea kuimarika kwakasi kubwa kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo.
Mkoa wa Arusha kwa mwaka 2018 umeweza kushika nafasi mbalimbali Kitaifa kama ifuatavyo;
-Darasa la nne nafasi ya 3 Kitaifa mwaka 2020
-Darasa la Saba nafasi ya 2 Kitaifa mwaka 2020
-Kidato cha Pili nafasi ya 1 Kitaifa mwaka 2020
-Kidato cha nne nafasi ya 1 Kitaifa mwaka 2020
Kidato cha Sita nafasi ya 6 Kitaifa mwaka 2020
Halmashauri zilizofanya vizuri 2020
Darasa la Nne
Halmashauri ya Jiji la Arusha ya kwanza katika Halmashauri Kitaifa
Darasa la Saba
Halmashauri ya Arusha Jiji ya kwanza Kitaifa
Halmashauri ya Arusha ya Nane katika halmashauri kumi bora Kitaifa
Kidato cha Pili
Halmashauri ya Arusha Jiji na Halmashauri ya Arusha zipo katika Halmashauri kumi bora
Kidato cha Nne
Halmashauri ya Meru imeingia kumi bora Kitaifa
Kidato cha Sita
Shule 3 zimeingia katika kumi bora
1.Kisimiri
2.Ilboru
3.Mwandet
Mkoa wa Arusha una jumla ya taasisi za kielimu 1,082 zinazotoa Elimu kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu. Kati ya hizo zipo shule za msingi za umma na za binafsi 757, Sekondari 240, vyuo vya ualimu 10, Vyuo vya ufundi stadi 52, vyuo vikuu 9 na Vyuo vinginevyo 14.
Katika kuimarisha sekta ya elimu Serikali imeendelea kutekeleza mikakati anuawai yenye lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza na pia mikakati yenye kuzilenga kaya maskini sana (poor of the poor). Hii ni pamoja na uanzishwaji wa shule mpya, ujenzi wa miundombinu ya elimu na upatikanaji wa vifaa, kuanzishwa kwa mpango wa elimu bila malipo na mpango wa elimu lipa kwa matokeo. Hatua zilizochukuliwa kupitia mikakati hiyo ni kama ifuatavyo:
Hadi kufikia mwezi Juni 2019 Serikali Mkoani Arusha imeweza kuongeza idadi ya shule za msingi kutoka shule 519 mwaka 2015 na kufikia shule 537 mwaka 2019, kukiwa na ongezeko la shule mpya 18 sawa na asilimia 3.5. Shule za msingi za binafsi zilizopo ni 245 na hivyo kufanya idadi ya shule zote kuwa ni 782.
Shule za Sekondari za umma zimeongezeka kutoka 142 mwaka 2015 hadi 155 mwaka 2019, kukiwa na ongezeko la shule mpya 13, sawa na asilimia 9.2. Shule za Sekondari za binafsi zilizopo ni 99 na kufanya Mkoa kuwa na shule za sekondari 254.
Mpango wa Elimu bila Malipo ni mahsusi katika kuhakikisha kuwa kila mototo wa Tanzania anapata fursa ya Elimu ya Msingi (hadi kidato cha Nne) bila vikwazo vya kiuchumi au kijamii. Chini ya Mpango huo, Serikali imetoa jumla ya Shilingi 78,283,011,450 kwa Mkoa wa Arusha kati ya mwaka 2016 na 2019 ikiwa ni wastani wa Shilingi bilioni 1.80 kwa mwezi. Matumizi ya fedha hizi ni pamoja na:
Kwa wastani, jumla ya wanafunzi 416,773 wamekuwa wakinufaika na Mpango wa Elimu bila Malipo kila mwaka.
Katika kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari Serikali imeendelea kuwekeza katika ujenzi wa maabara kwa masomo ya Bailojia, Fizikia na Kemia. Kutokana na sera hiyo Serikali Mkoani Arusha imeweza kuongeza idadi ya vyumba vya maabara kutoka 49 mwaka 2015 hadi kufikia maabara 364 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la maabara 315 sawa na asilimia 643!. Hivi sasa Serikali inaendelea na uimarishaji wa maabara hizo kwa kuhakikisha zinakuwa na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia.
Mkakati huu wa Serikali unalenga kutambua mchango unaotokana na juhudi za wananchi na pia kupanua wigo wa wao kushiriki katika kuimarisha sekta ya elimu nchini. Katika kutekeleza kipaumbele hiki, Serikali imetumia jumla ya TZS 1,575,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule za sekondari na shule za msingi ambapo jumla ya madarasa 78 na vyoo matundu 238 yamejengwa katika shule za msingi na madarasa 78 katika shule za sekondari.
Mpango wa Elimu wa Lipa kwa Matokeo ni utaratibu unaohusu upimaji wa ufanisi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kutumia vigezo muhimu vya kielimu kama urekebishaji wa ikama ya walimu, uingizaji wa takwimu za kielimu zilizo sahihi kwenye mfumo wa BEMIS (Basic Education Management Information System) na hivyo kuziwezesha kupatiwa fedha kulingana na ubora wa matokeo ya upimaji.
Tangu kuanza kwa Mpango huo mwaka 2015/2016 Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya Shilingi 5,765,713,767 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, mabweni, mabwalo, matundu ya vyoo na ukamilishaji wa miradi ya ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari na pia kulipa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri kwenye utendaji kazi wao.
Kati ya fedha hizo, jumla ya TZS 1,203,200,000 zimetumika kwenye shule za sekondari kwa shughuli za ujenzi wa ofisi za utawala 3, matundu ya vyoo 12, mabwalo 2, maktaba 2, mabweni 8, madarasa 9 na nyumba 1. Kiasi kilichosalia cha TZS 651,000,000 kilitumiwa na shule za msingi kujenga madarasa 20, matundu ya vyoo 66, bweni 1 na nyumba 3 za walimu.
Katika kuimarisha ufaulu wa wanafunzi katika ngazi zote za elimu ya msingi na sekondari, Mkoa wa Arusha umeanzisha Mpango maalum wa kufanya mitihani ya pamoja ya ndani ya kuwapima wanafunzi kwa shule zote kabla ya mitihani ya kitaifa. Utaratibu huu unaosimamiwa moja kwa moja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ambapo tathmini za awali zimeonyesha kuwepo kwa ari ya kufundisha, kwa mujibu wa syllabus miongoni mwa walimu ili kujihakikishia matokeo mazuri.
Mafanikio yaliyopatikana kutokana na juhudi hizo za Serikali ni pamoja na:
Kumekuwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wa ngazi mbalimbali za elimu hususan kutokana na mpango wa Serikali wa Elimu bila malipo:
Ongezeko la Kiwango cha Ufaulu
Maendeleo ya ufaulu wa wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu, kati ya mwaka 2015 na mwaka 2019 ni kama ifuatavyo:
Mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na:
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa