Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko pamoja na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda wakitembelea mabanda ya maonesho ya Karibu Kili-Fair 2025 katika Viwanja vya Magereza - Kisongo Jijini Arusha, maonesho yanayozinduliwa rasmi leo Juni 6, 2025.
Zaidi ya kampuni 500 kutoka nchi zaidi ya 40 zinashiriki maonesho hayo, yakilenga kutangaza vivutio vya utalii, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta hiyo muhimu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa