• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

DKT. SAMIA AMEBORESHA VIWANJA VYA NDEGE ARUSHA NA MANYARA KUKUZA UTALII NCHINI- RC MAKALLA...

Posted on: October 10th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.CPA Amos Gabriel Makalla amemshukuru Rais wa Serikali ya Awamu ya sita Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu ya Viwanja vya ndege vya Arusha na Manyara, lengo likiwa kupanua huduma za miruko ya ndege kwa saa 24 pamoja na kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma kwa abiria hususani watalii.


CPA Makalla amesema hayo leo Oktoba 10, 2025, alipoungana na Menejimenti ya Uwanja wa Ndege Arusha pamoja na watoa huduma kwenye kiwanja hicho, ikiwa ni maadhimisho ya kilele cha Wiki ya huduma kwa Wateja iliyoanza 6 - 10 Oktoba, 2025 huku akiipongeza Menejimenti ya Uwanja huo, kwa kuendelea kutoa huduma bora sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege ambao umekuwa chachu ya ongezeko la watalii mkoani humo.


 "Dkt. Samia amekuwa na dhamira ya dhati ya kukuza utalii kwa kuhakikisha viwanja vinakuwa na miundombinu rafiki itakayowezesha kufanya kazi kwa saa 24 na kuruhusu kutua ndege kubwa, jambo ambalo linaimarisha sekta ya uchukuzi sambamba na kukuza utalii na uchumi wa Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla". Amefafanua CPA Makalla.


Ameongeza kuwa, licha ya Filamu ya Royal Tour kuvutia na kuongeza idadi ya watalii nchini, mkoa wa Arusha ni miongoni mwa eneo ambalo linanufaika kwa ongezeko kubwa la idadi ya watalii wanaoingia na kuwataka watoa huduma kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa wageni na kuondoa kero kwa abiria.

Hata hivyo, amewataka watumishi na wadau wanaotoa huduma kwenye uwanja huo, kutambua kuwa wanayo dhamana ya kukuza utalii nchini kwa kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wateja, huduma ambazo ndio chachu ya maendeleo ya uchumi na kukuza sekta ya utalii.


"Management ya Arusha Air Port imechangia kwa kiasi kikubwa Makampuni ya utalii kufanya kazi vizuri kwa ushindani na kuhakikisha watalii wanapata huduma bora na kwa wakati,  jambo ambalo linaongeza chachu ya maendeleeo na ukuzaji wa uchumi kupitia sekta ya utalii nchini, hii inaonesha dhana kubwa ya kuwaamini vijana katika kazi" Amebainisha.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKALLA AWAONYA TATU MZUKA WANAOPORA WANANCHI ARUSHA..

    October 13, 2025
  • MIRADI YA STENDI, SOKO NA JENGO LA UTAWALA JIJI LA ARUSHA IKAMILIKE KWA WAKATI- RC MAKALLA..

    October 13, 2025
  • TAMISEMI YA SAMIA; MAFANIKIO YANAONEKANA...

    October 10, 2025
  • DKT. SAMIA AMEBORESHA VIWANJA VYA NDEGE ARUSHA NA MANYARA KUKUZA UTALII NCHINI- RC MAKALLA...

    October 10, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa