_Wengi hatarini kufia usingizini_
Watu takribani 600 wamegundulika kuwa na matatizo mbalimbali ya moyo kati ya watu 1500 waliohudumiwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho kikwete kwenye kambi maalum ya matibabu ya kibingwa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Peter Kisenge wakati alipokuwa akitoa tathimini ya huduma za taasisi hiyo wakati wa kambi hiyo ya matibabu ya siku nane inayotarajiwa kumalizika Jumatatu ya wiki ijayo.
Daktari huyo bingwa wa magonjwa ya moyo mesema miongoni mwa magonjwa ya moyo yenye kuwasumbua wananchi wengi wa Arusha ni pamoja na moyo kuwa dhaifu kwa kushindwa kufanya kazi zake kikamilifu suala ambalo limekuwa likisababisha vifo vya ghafla wakati mtu akiwa usingizini.
Katika hatua nyingine pia amesema jumla ya watoto 150 walipimwa na kupatiwa matibabu na Taasisi yake ambapo kati yao watoto 53 wamegundulika kuwa na matatizo ya valvu kwenye moyo na hivyo kuhitaji upasuaji mkubwa Jijini Dar Es salaam.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa