Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Athumani Kihamia amewataka wachimbaji wa madini ya ujenzi kuzingatia sheria ili kulinda mazingira ya maeneo ya machimbo.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa wachimbaji wa madini ya ujenzi kwa Mkoa wa Arusha.
Uchimbaji wa madini ya ujenzi kiholela ndio unasababisha uwaribifu wa mazingira kama vile kuaribu misitu na barabara.
Amesisitiza pia mashimo yanayoachwa wazi yanatunza Maji ambayo yanageuka kuwa mazalia ya mbu.
Amewataka wachimbaji hao wa madini ya ujenzi kufuata mfumo rasmi wa kuwa na leseni maalumu ya uchimbaji.
Dkt. Kihamia amesema kufuata utaritibu huo utasaidia hata nchi kupata mapato yaliyo halali.
Nae, Meneja wa Baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini bwana Lewis Nzari amewataka wachimbaji wa madini ya ujenzi kuacha kufanya shughuli zao usiku badala ya mchana ili kuwa na usalama zaidi wa maisha yao.
Amesema lengo la mafunzo hayo nikutoa elimu kwa wachimbaji hao juu ya uchimbaji wa madini ya ujenzi kwa njia iliyo bora na salama kwao.
Uchimbaji usio salama kwao umesababisha kuwa na vifo katika machimbo hayo na uwaribifu mkubwa wa mazingira hasa Barabara kuaribiwa.
Kikao cha utoaji elimu ya uchimbaji bora wa madini ya ujenzi kilijumuisha wataalamu mbalimbali wa mazingira na viongozi wa wachimbaji madini ya ujenzi kwa Mkoa wa Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa