Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, wametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madaras shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza Maasai, iliyopo mtaa wa Korongoni Kata ya Lemara, Jiji la Arusha, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta ya Elimu leo Februari 26, 2024
Jengo hilo lenye ghorofa mbili, likitekelezwa kwa awamu, likijumuisha ujenzi wa vyumba 16 vya madarasa na matundu 44 ya vyoo huku kila sakafu ikiwa na vyumba vinne vya madarasa na tayari sakafu ya chini imekamilika.
Lengo la mradi ni Kuboresha miundo mbinu ya EElim kwa shule za Msingi ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani katika shule zetu zinazotoa elimu kwa mfumo wa lugha ya Kingereza
Mradi huo unatekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani ya na unategemea kugharimu shilingi milioni 760, milioni 400 ni fedha kutoka Serikali Kuu na milioni 365 ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji.
Shule hiyo ilisajiliwa rasmi mwaka 2023 kwa namba ya usajili EM.20187ikiwa na jumla ya wanafunzi 106 kwa darasa kwanza na awali, wavulana 48 na wasichana ni 58 ambao
wanatumia vyumba 4 vya mamadara vilivyokamilika na matundu 11 ya vyoo .
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa