TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEKELEZAJI NA MAFANIKIO YA SHUGHULI ZA SERIKALI MKOA WA ARUSHA JANUARI HADI DISEMBA 2017
UTANGULIZI
Mkoa wa Arusha ni moja kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara, wenye ukubwa wa Km za mraba 34,515.5. kiutawala Mkoa unao Wilaya sita Halmashauri 7, Tarafa 23, Kata 33, Vijiji 393, mitaa 154 na vitongoji 1471.
Idadi ya watu kwa ongezeko la 2.7% kwa mwaka inakadiriwa kufikia jumla ya watu wapato 1,835,787 wanawake wakiwa 51.5% na wanaume 48.5%.
UCHUMI
Shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Arusha hasa hasa za kilimo na wafugaji ambao huchangia 20%, biashara huchangia 10.9%, viwanda na sekta nyingine huchangia 15.5%.
Pato la Mkoa limefikia Tsh. Trilion4,876, ambalo huchangia asilimia 4.77 kwenye pato la Taifa. Pato la Mkoa kwa mwaka ni (per capital income Tsh. 2,576.517).
HALI YA USALAMA
Hali ya ulinzi na usalama ya Mkoa ya Mkoa wa Arusha ni ya kuridhisha hasa baada ya juhudi kubwa kuwekwa na vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti mianya ya matuko yanayosababisha uvunjivu wa Amani. Wananchi wameendelea na shughuli za uzalishaji mali na kukuza kuhusu bila hofu yoyote ya usalama wao wa mali zao.
TAARIFA ZA SEKSHENI NA VITENGO
MAFANIKIO
Sekta ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji
Mkoa wa Arusha ni moja ya Mikoa iliyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya viwanda hapa nchini. Kuna Viwanda Vikubwa 38, vya Kati 131 na Vidogo 2165 vinatoa ajira zaidi ya 50,000 na vinachangia asilimia 10.9 ya pato la Mkoa.
Serikali kupitia Programu ya MIVARF imejenga ghala la kuhifadhi vitunguu kwa ajili wa wakulima wa zao hilo pamoja na miundombinu ya ya barabara katika Tarafa ya Eyasi, Wilaya ya Karatu. Mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi za kitanzania 1,530,450,036/- ambayo asilimia 95 ni ya Mradi na asilimia 5 ni ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu uwezo wa kuhifadhi vitunguu hadi tani 2400.
Mradi huu tayari umekamilika na tayari wakulima wote wanaendelea kuhifadhi vitunguu na kuanzia tarehe 1/12/2017 shughuli zote za biashara ya vitunguu zimeanza kufanyikia ndani ya eneo la Ghala hilo kama soko pekee kwa ajili ya kuendeshea shughuli ya biashara ya vitunguu.
Wakulima wameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kondoa kero iliyodumu kwa muda mrefu ambapo kulikuwa na wavamizi kutoka Nchi jirani katika mashamba yao ambapo walikuwa wakinunua mazao yangalipo mashambani kwa bei waliyoamua wao. Tangu kujengwa kwa mradi huo, bei ya vitunguu imeongezeka kutoka TSh. 40,000 Kwa gunia hadi Tsh 100,000 kwa gunia baada ya mradi, baada kuhifadhiwa katika ghala hilo na kuuzwa katika soko halali linaloendeshwa eneo hilo la ghala.
Pamoja na mafanikio Serikali imegundua bado kuna matumizi yasiyo sahihi ya vipimo hivyo inahitajika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo ili wakulima wasiendelee kupunjwa na Serikali kukosa mapato halali
Sekta ya Mifugo
Ujenzi wa Soko la kisasa la mifugo
Ujenzi wa Soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Eworendeke Wilayani Longido ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi chini ya Programu ya MIVARF. Ujenzi huu umegharimu kiasi cha Tsh. 782,050,572 ambayo asilimia 95 ni ya Mradi na asilimia 5 ni ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Uwepo wa Soko hili utasaidia kupunguza kero ya utoroshwaji wa mifugo kwenda Nchi jirani, kuongeza uzalishaji wa Mifugo na mazao yake kutokana na uwepo wa uhakika wa soko la mifugo. Pia kuboresha na kuinua kipato cha wananchi kwa kuuza mifugo ndani ya Tanzania na Nchi jirani, ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuipatia Serikali mapato ambayo yalipotea kwa muda mrefu kutokana na utoroshwaji wa mifugo kwenda nchi jirani.
Aidha, uwepo wa soko hili utasaidia kuhifadhi mazingira yaliyokuwa yanaharibiwa na mifugo waliokuwa wakitoroshwa kwa kuswagwa kupitia njia zisizo rasmi kwenda Nchi jirani.
Sekta ya Maliasili Na Utalii Na Uhifadhi Wa Mazingira
Kuondolewa malango ‘Gates’ ukanda wa ziwa Natroni
Sekta ya Utalii imekumbwa na changamoto ya muda mrefu wa uwepo wa Mageti katika ukanda wa Ziwa Natroni ambapo mageti yalikuwa yamewekwa kila mpaka wa Halmashauri za Wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro. Mwaka 2017/2018 Mkoa kupitia Mhe. Mkuu wa Mkoa umefanya jitihada za Kuhakikisha keKuondolewa malango ‘Gates’ matatu ambayo yalikuwa kero kwa wageni “Tourists” mwelekeo wa ukanda wa Ziwa Natroni katika Halmashauri za Wilaya ya Monduli, Longido na Ngorongoro. Baada ya jitihada mbalimbali yalifikia kubakisha lango moja linalokusanya mapato kwa ufanisi.
Kumekuwa na ongezeko la wageni/watlii wanaotembelea vivutio (“Number of Visitor Arrivals”) ambapo mwaka 2016 watalii 1,284,279 na "projection" kwa mwaka 2017 ni 1,436,480 na inatarajiwa kuongezeka. Aidha, asilimia 80 ya Watalii wanaofika Tanzania hufika/kupita Mkoa wa Arusha.
Mapato yatokanayo na Utalii yamekuwa yakiongezeka kutoka trilioni 3.71 mwaka 2015 hadi trilioni 4.64 Mwaka 2016; Aidha, mapato yanakadiriwa kuongezeka kwa kulinganisha mapato ya mwezi Januari – Novemba, 2017 NCAA na TANAPA pekee, Jedwali Na. I: limeainisha takwimu za mapato kitaifa kwa mwaka 2015 & 2016 na mapato ya Januari - Desemba, 2017 ya NCAA na TANAPA. Mapato mengine ya Utalii yanatokana na Utalii wa Picha, Utalii wa Uwindaji na Utalii wa Utamaduni na (WMA).
Jedwali Na. I: Takwimu za mapato kitaifa kwa mwaka 2016 & 2017, pia mapato ya Mwezi Januari – Novemba, 2017 kwa upande wa NCAA na TANAPA.
MWAKA |
MAPATO KITAIFA |
TANAPA |
NCAA |
2016
|
Trilioni 4.64
|
- |
- |
Januari-Novemba, 2017
|
- |
138.7bilioni
|
- |
Januari - , 2017
|
- |
- |
65.6bilioni
|
2015 - 2016
|
Ongezeko;
Bilioni 87 |
- |
-
|
Chanzo: Kitabu cha Takwimu za Utalii cha Wizara ya Maliasili na Utalii, Idara ya Utalii, Mwaka 2016 ; NCAA & TANAPA, 2017
Mradi wa Kukabilinana na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Kwa muda wa zaidi ya Mikaka 10 Mkoa wa Arusha umekwa ukikabilia na mtawanyiko hafifi ambao umesababisha upungufu wa maji, malisho na na hata kusababisha mifugo kufa na upungufu wa uzlishaji wa mazo ya chakula na biashara. Serikali kwa kushikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali IIED na Hakikazi Catalyst wametekeleza kwa kasi Miradi 34 ambayo inagharimu Tsh. 1,908,015,342 kwa ajili ya kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi katika Halmashauri Za Wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro.
Baraza la Uwezeshaji
Mafanikio ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Katika Mkoa Wa Arusha Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Makundi ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu ni muhimu katika ujenzi wa Taifa letu hususan katika Nyanja ya uchumi. Ili kufikia uchumi wa kati unaotegemea tasnia ya viwanda Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuongeza makusanyo ya ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hali iliyopelekea ongezeko kubwa la idadi ya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu kunufaika mikopo ya 10% inayotengwa kwenye makusanyo ya ndani. Aidha, uwezeshaji kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu katika mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa ni jumla ya Tshs. 2,554,500,000/= kwa vikundi 279 vya vijana na vikundi 370 vya wanawake. Ambapo vijana Tshs. 1,059,000,000/= na wanawake Tshs. 1,495,500,000/= ikiwaazma kubwa ni kuongeza ushiriki wa shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali katika makundi haya muhimu ya ujenzi wa Taifa.
Mkoa unaendelea kumuunga mkono Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, juhudi za kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali kwa kuzindua Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Aidha, majukwaa 116 yamezinduliwa katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata, ambapo jukwaa 1 la Mkoa, majukwaa 7 ya Halmashauri na majukwaa 108 yaKata kati ya Kata 158 yakiwa na lengo kuu la kuelimisha nguzo tisa za Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004. Hali iliyopelekea Mkoa kupata tuzo ya Taifa ya uwezeshaji, kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Mikoa 26 ya Tanzania Bara katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Sekta ya Ushirika
Vyama vya Ushirika 12 vya walaji (Consumers) vimeandikishwa katika Tarafa ya Ngorongoro. Lengo ni kusaidia wananchi kuapata bidha/chakula kwa urahisi na bei nafuu ili kuweza kukabilina na hali ya ukame.
Jitihada za kuondoa kero ya upatikanaji MAJI:
Maji vijijini.
Usimamizi wa Huduma za maji katika makao makuu ya wilaya:
HALMASHAURI |
MAKISIO |
MAKUSANYO |
ASILIMIA |
ARUSHA CC
|
12,299,585,000 |
13,603,884,903 |
111% |
ARUSHA DC
|
3,200,600,000 |
2,944,941,862 |
92% |
MERU DC
|
3,627,024,000 |
3,411,094,173 |
94% |
LONGIDO DC
|
1,343,549,980 |
904,070,011.17 |
67% |
KARATU DC
|
3,887,383,000 |
2,731,081,486 |
70% |
NGORONGORO DC
|
2,094,282,000 |
1,542,484,157 |
74% |
MONDULI DC
|
2,415,317,000 |
2,210,120,822 |
90% |
JUMLA |
28,909,733,983 |
27,347,677,414 |
95% |
HALMASHAURI |
MAKISIO |
MAKUSANYO |
ASILIMIA |
ARUSHA CC
|
14,580,000,000.00 |
5,976,702,539.00 |
40.99 |
ARUSHA DC
|
3,493,318,000.00 |
1,304,011,053.00 |
37.33 |
MERU DC
|
3,710,623,000.00 |
1,465,110,295.00 |
39.48 |
LONGIDO DC
|
1,039,747,000.00 |
519,552,217.00 |
49.97 |
KARATU DC
|
2,211,206,000.00 |
906,180,470.00 |
40.98 |
NGORONGORO DC
|
4,177,604,000.00 |
1,268,922,171.00 |
30.37 |
MONDULI DC
|
2,429,883,000.00 |
738,437,080.00 |
30.39 |
JUMLA |
31,642,381,000 |
12,178,915,825 |
38.49 |
HALMASHAURI |
MWAKA 2014/15 |
MWAKA 2015/2016 |
ARUSHA CC
|
Hati inayoridhisha |
Hati inayoridhisha |
ARUSHA DC
|
Hati inayoridhisha |
Hati inayoridhisha |
KARATU DC
|
Hati isiyoridhisha |
Hati yenye mashaka |
LONGIDO DC
|
Hati yenye mashaka |
Hati yenye mashaka |
MONDULI DC
|
Hati inayoridhisha |
Hati inayoridhisha |
MERU DC
|
Hati yenye mashaka
|
Hati inayoridhisha |
NGORONGORO DC
|
Hati yenye mashaka |
Hati inayoridhisaha |
SEKRETARIET YA MKOA
1.Ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote 7 umefanyika, na jumla ya miradi 398 kati ya miradi 613 iliweza kukaguliwa kwa kipindi cha Julai hadi Juni 2016/2017.
Seksheni pia imeweza kukagua miradi 125 ya mwaka wa fedha 2017/2018 na mingi ya miradi hii ipo katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Barabara. Utekelezaji wa miradi hii upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na baadhi ya miradi imekamilika ikiwemo miradi ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu (6 in one), mabweni ya wanafunzi, ujenzi wa vituo vya afya, Zahanati na baadhi ya miradi ya Maji Vijijini
2. Uanzishwaji wa jukwaa la wanawake la Mkoa wa Arusha limeanzishwa na sasa wanawake wa mkoa wa Arusha wanazo fursa mbalimbali za kutumia jukwaa hili katika kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha biashara mbalimbali na kupata fursa ya kuunganishwa katika mtandao wa taasisi za kifedha zitakazoweza kuwakopesha kwa riba nafuu sana
3. Kwa upande wa programu ya TASAF III na OPEC III mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na
- Mpango wa kunusuru kaya maskini ambapo katika Mkoa wa Arusha Jumla ya Kaya maskini 62,492 zikiwa na wanaume 5,059 na wanawake 41,771 zimeweza kutambuliwa baada ya kukidhi viegezo.
- Jumla ya fedha Tshs 22,652,188,870.37 zilipokelewa katika Mkoa wa Arusha toka TASAF Makao Makuu kwa ajili ya malipo ya Kaya maskini zipatazo 46,771 katika Vijiji na Mitaa 290 tangu awamu ya kwanza ya mpango huu Julai hadi Agasti 2015
- Mkoa umefanikiwa kutekeleza miradi 63 ya ujenzi wa miundombinu mbalimabali ya Jamii, ikiwemo miradi ya sekta ya elimu, Afya, Barabara, mifereji ya umwagiliaji na mazingira, yenye thamani ya Tshas 2,748,468,978.39 (miradi 9 kwa kila Halmashauri ya Wilaya)
Uandikishaji wa wanafunzi wa kuanza Elimu ya awali na darasa la kwanza hadi Desemba 2016 ulikuwa wanafunzi 88,268 lakini hadi kufikia Desemba 2017, hali ya maoteo ya uandikishaji wa elimu ya Awali ni wanafunzi 102,411 (wav 52,142 was 50,269).
Mkoa umekuwa na ongezeko la madarasa ya Elimu ya Awali kutoka 647 Desemba 2016, hadi kufikia 715 Desemba, 2017 sawa na ongezeko la 9.23% shule za msingi 690 Desemba, 2016 hadi shukle za msingi 723 Desemba, 2017 sawa na ongezeko la 4.56% sekondari 230 Desemba, 2016 hadi shule 213 Desemba 2017 sawa na ongezeko la 0.43%.
Uchaguzi wa wanafunzi wa kuanza kidato cha kwanza hadi kufikia mwezi Desemba, 2016 ulikuwa ni wanafunzi 26,984(wav 12,583 was 14,401) sawa na 100% ya wanafunzi wote waliofaulu. Uchaguzi wa wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza Januari, 2017 ni 29,624(wav 14,215, was 15,409) ongezeko la wanafunzi 2,640. Wanafunzi wote waliofaulu sawa na100% wamepata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza 2018.
Hadi Desemba, 2016 Mkoa ulikuwa na jumla ya shule 118 ambazo zilikuwa hazijasajiliwa na zilikuwa zinaendeshwa kinyume cha sheria ya Elimu Na. 24 ya mwaka 1978 na marekebisho yake ya 1995 na 2002. Lakini hadi kufikia Desemba, 2017 shule zote (BUBU) zisizo na usajili zimefungwa na wanafunzi wamehamishiwa kwenye shule zenye usajili.
Hadi kufikia Desemba, 2016 Mkoa kupitia Halmashauri zake haukuwa na mradi wowote chini mpango wa Lipa kwa Matokeo (P4R) lakini katika kipindi cha mwaka mmoja hadi Desemba 2017 Mkoa ulipokea Tsh. 1,036,000,000/= kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya shule mpya za kidato cha Tano za Mwandeti, Mlangarini, Nainokanoka na Loliondo na kila shule ilipewa Tsh. 259,000,000/= za ujenzi wa madarasa, maabara, bweni moja na matundu ya vyoo umekamika 100%. Ujenzi bweni la pili umekamilika kwa 20%.
Mdondoko wa wanafunzi (Drop out) wa shule za msingi umepungua kutoka 18% Desemba 2016 hadi kufikia 16% Desemba 2017 kwa wanafunzi walioanza darasa la kwanza ikilinganishwa na waliomaliza darasa la Saba 2017. Lengo ni kuhakikisha mdondoko unapungua chini ya 10% mwaka 2018 na hatimaye kumalizika kabisa.
Kupitia Mpango wa Elimu bila Malipo, shule za msingi na Sekondari zimeendelea kupokea wastani wa Tsh. 1,842,990,926/= kwa mwezi ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji wa shule ambapo shule za msingi zinapokea Tsh. 620,091,380/= na shule za sekondari zinapokea Tsh. 1,222,899, 546/=.
Hadi kufikia Desemba 2017 serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari na msingi maalum kwa watoto wenye mahitaji maalum. Gharama ya mradi huo ni Tsh. 4.5 bilion na awamu ya kwanza zimepokelewa Tsh. 1.2 bilioni na ujenzi unaendelea. Lengo ni kuhakikisha ujenzi umekamilika 2018.
Desemba 2016 vijana 200 waendesha pikipiki (bodaboda) walipewa mkoa wa pikipiki 200 usio na riba zenye thamani ya Tsh. 400,000,000/=. Kufikia tarehe 27 Desemba, 2017 kiasi cha Tsh. 284,851,644/= kimekwisha rejeshwa sawa na66.7% ya marejesho yote ambayo ni Tsh. 427,140,000/=. Wastani wa vijana waliorejesha ni 133.4 kati ya vijana 200 na wastani wa vijana ambao hawajarejesha ni 66.6 tu sawa na 33.3% kati ya vijana 200. Baada ya kukamilisha marejesho yote Tsh. 200,000,000/= zitabaki kama mtaji kwa vijana hawa na Tsh.200,000,000/= matarajio ya fedha zilizobaki kwa mwaka 2018 ni kuzielekeza kwa akina mama wamachinga kama mkopo ya mitaji isiyokuwa na riba.
Katika sekta ya miundombinu mambo muhimumatano (5) yaliyoshughulikiwa ni pamoja na:-
Hivi sasa serikali imeshatolea maelekezo ya namna ya utatuzi ikiwa ni pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuandaa Muswada wa sheria utakowasilishwa serikalini kupitia Baraza la Mawaziri kuhusu sheria Mahsusi ya eneo la Loliondo.
Aidha katika kutatua migogoro ya ardhi katika Jiji la Arusha jumla ya viwanja 163 vimetolewa kwa wananchi waliokuwa wanadai fidia ya viwanja mbadala katika eneo la Oljoro.
Mkoa kupita Wilaya zake umehimiza kutenga maeneo ya uwekezaji na viwanda na bandari kavu ambapo mpaka hivi sasa jumla ya ekari 215,488.8 zimetengwa kutoka ekari 111,203 mwaka 2016 sawa na ongezeko asilimia 93.7.
Aidha malengo kwa mwaka 2018 ni kuhakikisha maeneo hayo yanawekewa miundombinu na kuhamasisha wawekezaji na kuendelea kutenga maeneo mapya. Maeneo yaliyotengwa kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:-
Upimaji wa maeneo ya Taasisi za Umma, umeongozeka kutoka maeneo 62 mwaka 2016 hadi 134 mwaka 2017 ongezeko lamaeneo 72 sawa na asilimia 116.
(B) SEKTA YA BARABARA
MAFANIKIO USAFI WA MAZINGIRA
Kwa mwaka 2017 Mashindano yalifanyika kote nchini kwa kushirikisha ngazi ya Halmashauri za Wilaya,Manispaa, miji, Majiji, vijiji,Hospitali za Rufaa za Serikali na za binafsi pamoja na Hotel zenye hadhi ya nyota tano.
Mkoa ulifanya vizuri na kushinda tuzo zifuatazo:-
USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI NA ZA SERIKALI (PPP)
Mkoaunatambua mchango mkubwa wa Wadau katika kuboresha huduma za Afya katika Halmashauri zetu na kukabiliana na majanga mbalimbali.
Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa Afya Leopard Tours and Safaris’ waliweza kukarabati jengo la kupimia wingi wa Virusi vya UKIMWI (Viral Load)katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambalo limeshaanza kutoa huduma hivyo na kupelekea wagonjwa wanaotumia dawa kujua matokeo mapema na kupunguza gharama za usafirishaji wa sampuli kwenda KCMC. Mkoa pia unapokea sampuli kutoka Mikoa jirani ya Manyara na Singida. Hadi kufikia Desemba, 2017 idadi ya wagonjwa wa UKIMWI waliopimwa kwa kutumia vipimo vya Viral Load.
Uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu
Kupitia ufadhili wa NTLP,Mkoa umeweza kuchagua Maduka ya dawa binafsi na kuyajengea uwezo wa kutambua dalili za mwanzo za kifua kikuu ili kuwapa rufaa kwenda kwenye maabara binafsi zilizoteuliwa kupima makohozi kwa lengo la kuongeza kasi ya kuibua wagonjwa wa Kifua kikuu mapema. Jumla ya maduka 13 na maabara 5 zinatoa huduma hiyo.
Kupitia ufadhili wa KNCV,Mkoa umefanikiwa kuongeza uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu mfano wamefanikiwa kuweka darubini ya kisasa (LED-Fluorence Microscopy) katika Halmashauri ya Longido na kupekelea kuongeza idadi ya wagonjwa kutoka 14 mpaka 61.Pia wameweka machine ya kisasa yenye uwezo wa kugundua vimelea vya kifua kikuu na usugu wa dawa za kifua kikuu (GXP-GeneXpert) amabayo imeweza kuibua wagonjwa wengi zaidi.
HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO
A: Ukarabati wa vyumba vya cPAC
UUNDWAJI WA TIMU YA URATIBU WA AFYA MOJA “ONE HEALTH COORDINATION TEAM”
Mkoa wa Arusha umefanikiwa kuanzia Timu ya Afya moja (One health coordination team) inayoshirikisha sekta mbalimbali katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali mfano magonjwa yanayoweza kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kama kimeta, magonjwa yanayohusisha maji kama kipindupindu na majanga mengine yanayosababisha madhara kwa afya ya binadamu. Tumefanikiwa kuelimisha jamii kuhusiana na magonjwa ya mifugo yanayoenezwa kwa binadamu, kuchukua sampuli 27 za binadamu kwa uchunguzi wa maabara wa kimeta ambapo 7 zilithibitishwa. Pia Mkoa umefanikiwa kutoa chanjo kwa mifugo 405,462(7%) kati ya mifugo 5,760,329.
UTOAJI WA TAARIFA YA MAGONJWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
Mkoa wetu umefanikiwa kutuma ripoti kwa ukamilifu kwa wastani wa asilimia 94 na kwa wakati asilimia 75 kwa mwaka 2017.
TAARIFA YA MAFANIKIO YA TAKWIMU (MTUHA)
Tumefanikiwa kushika nafasi ya nne ngazi ya Kitaifa katika uingizaji wa takwimu kwa wakati na usahihi (Jan-Jun 2017)
Mkoa umefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika utoaji wa taarifa za mwenendo wa kulaza wagonjwa (Bed Occupancy) kwa wakati na usahihi kwa mwaka 2017
MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU
Ununuzi wa mashine ya kisasa ‘’Ultra-Modern Ultra sound with Dopler’’
Mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa Afya kutoka Netherland wameweza kuinunulia Hospitaliya Mkoa ya Mount Meru ‘’Ultra-Modern Ultra sound with Dopler’’ yenye thamani ya Tsh.40,000,000/= ambapo inapima vipimo vifuatavyo:-
Magonjwa na mapungufu mbalimbali ya mishipa ya damu (Deep Venous thrombosis)
Kusinyaa kwa mishipa ya damu (Atherosclerosis)
Upimaji wa matiti (Uvimbe na saratani)
Kupima viungo vyote vya ndani ya mwili
Kupima hali ya ubongo kwa watoto baada ya kuzaliwa.
Kutokana na mashine hii, Hospitali yetu imeweza kupunguza kutuma wagonjwa nje kutafuta vipimo hivyo na kuongeza idadi ya wagonjwa wanaohitaji vipimo hivi kutoka nje ya Hospitali. Vile vile tumeweza kuongeza mapato kutoka shilingi 1,228,587,852/= (2015/16) hadi 1,776,564,311 (2016/17) sawa na ongezeko la 45%.
Mambo Matano ya ufanisi katika Kitengo Cha Ukaguzi wa Ndani – Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha ni yafuatayo;
Mafanikio katika mwaka 2017 kitengo cha TEHAMA.
Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na vituo vya afya mapato yameongezeka kwa marambili zaidi ukilinganisha na kipindi cha awali kabla ya kutumia mfumo.
Tangu Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Novemba 2015 imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 – 2020, kama Mkoa mambo mengi yatatekelezwa katika kuinua uchumi, ujenzi wa miundombinu, uboreshaji wa huduma za Afya, Elimu, Ukusanyaji wa mapato na utumiaji sahihi wa mapato ya Serikali.
Lengo ni kumsaidia mwananchi mnyonge na kuboresha maisha ya jumla ya wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Jukumu la wananchi ni kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli na wasaidizi wake wote.
MRISHO MASHAKA GAMBO
MKUU WA MKOA
ARUSHA
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa