• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MAONYESHO YA TATU YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA 2023; KUFANIKA MKOANI ARUSHA...

Posted on: November 19th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Maonesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa 2023, yanafanyika mkoani Arusha, kuanzia kesho, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini,  Arusha.

Akizungumza na Wandishi wa Habari leo, Kamishna wa Idara ya Uendeshaji Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, amesema kuwa Maonesho hayo yatafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 20 - 26 Novemba, 2023 na kuwataka wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani, kufika kwenye maonesho hayo.

Amesema kuwa lengo la Wiki ya Huduma za Kifedha ni kutoa elimu kwa Umma, juu ya Huduma za kifedha na kuwa na uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma rasmi za kifedha, zitakazosaidia katika kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.

"Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 - 2029/30, Elimu kwa Umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo" Amesema Dkt. Mwamwaja

Ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuboresha mazingira rafiki ya huduma za kifedha, na mpaka sasa asilimia 53.8 ya watanzania hutumia huduma rasmi za kifedha, ikiwa bado idadi kubwa ya watanzania hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha, hivyo utoaji wa elimu kwa Umma utasaidia, wananchi kuacha kutumia mifumo isiyo rasmi ya kifedha na kufikia lengo la Serilaki la asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

Naye Meneja msaidizi wa Mawasiliano, Benki kuu ya Tanzania, Noves Mosses, amesema Benki  hiyo ni msimamizi wa taasisi zingine za kifedha, iliyojikita kutoa elimu kwa Umma, ili kuwa na uelewa mpana kwenye masuala ya huduma za kifedha ili  kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi
kutembelea kwenye mabanda, yaliyopo kwanye Uwanja huo wa Maonesho na kuwasisiza, wananchi wenye wenye changamoto au kuhitaji kupata ufafanuzi na utatauzi wa changamoto hizo, kwa kuwa huduma zote zitatolewa bure,
 
Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika,  kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika mko wa Arusha, Grace Msambaji, amesema vyama vya ushirika humwinua mnyonge kutoka chini, na kuwa wamejipanga kuwahudumia wananchi katika kuendeleza uchumi wa watanzania.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa