• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MIKOPO YA ASILIMIA 10 KUANZA KUTOLEWA KABLA NOVEMBA 30, 2024..

Posted on: October 30th, 2024

MIKOPO YA ASILIMIA 10 KUANZA KUTOLEWA KABLA NOVEMBA 30, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange amesema mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 itikanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri kwaajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza kutolewa kabla au ifikapo Novemba 30, 2024 ili kuweza kuwanufaisha walengwa wa mikopo hiyo.

Mhe. Dkt Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Santiel Eric Kirumba Mbunge wa Viti Maalum aliyeuliza Je, lini Serikali itarudisha mikopo ya asilimia 10 kwa Makundi Maalum.?

Amesema mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ilisitishwa tarehe 13 Aprili, 2023 ili kupitia na kuboresha utaratibu wa utoaji wa mikopo hiyo kutokana na changamoto zilizobainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Mwaka wa Fedha 2021/22.

“Serikali imekwisharekebisha sheria na imeshapitia Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2019 na marekebisho yake ya mwaka 2021 na kutoa Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2024.”

Aidha Dkt. Dugange ameongeza kwa kusema kuwa shughuli zilizoanza kutekelezwa ni kutoa mafunzo kuhusu mfumo mpya wa utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo kwa wasimamizi 862 katika ngazi ya mikoa na halmashauri. Aidha, mafunzo yanaendelea kutolewa kwa kamati za usimamizi za huduma za mikopo ngazi za kata, halmashauri na wilaya pamoja na vikundi.

“kufuatia mafunzo yaliyotolewa uchambuzi wa awali wa mikopo umeshaanza katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na mikopo hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa kabla au ifikapo tarehe 30 Novemba, 2024.” Dkt. Dugange.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa