Mkoa wa Arusha utatumia matokea ya mtihani wa Moko kwa kidato cha nne kama ishara ya kufahamu kiwango cha ufaulu kwa mtihani wa Kitaifa na hii itasaidia kufanya maandalizi mapema.
Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akipokea mifuko 300 ya siment kutoka kwa Molvaro Logdes and Tented camps itakayosaidi katika ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza kwa halmashauri ya Longido,Monduli na Arumeru.
Amesema kipaombele cha kwanza kwa Mkoa wa Arusha ni Elimu na ndipo vinafuata vingine kama vile Afya, Miundombinu na Madini, kwa kuliona hilo Mkoa ukaamua kuongeza nguvu zaidi katika ujenzi wa madarasa ili hadi kufikia mwisho wa mwezi Februari,2019 wanafunzi wote waliofaulu wawe wameshaanza masomo yao.
Gambo amesema katika mifuko hiyo 300 ya siment kila Wilaya itapata mifuko 100 kwa wilaya hizo tatu na simenti hiyo ikatumike kama ilivyopangwa kwa ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza.
Akikabidhi mifuko hiyo Mtendaji Mkuu wa Molvaro Lodges Mwalimu Musa amesema,sababu kubwa iliyoisukuma kampuni kutoa mifuko hiyo ni uhitaji mkubwa wa madarasa kwani wanafunzi wengi wamefaulu kuingia kidato cha kwanza.
Amewasii hata makampuni mengine nao kuchangia zoezi hili la ujenzi wa madarasa kwani jamii wanazoishi zinawasaida kwa kiasi kikubwa katika huduma zao kwani wote wanaishi kwa kutegemeana.
Akitoa shukrani za dhani kwa Mkuu wa Mkoa na kampuni ya Molvaro mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisombe,amesema mifuko hiyo 100 ya simenti itasaidia sana katika ujenzi wa madarasa kwani wilaya yake ilikuwa na iwitaji wa madarasa 16 na mpaka sasa wameshajenga 9, hivyo simenti hiyo itasaida zaidi kumalizia madarasa yaliyobaki.
Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru Mwalimu James Mtembe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro ameshukuru kwa wilaya yake kukumbukwa katika mgao huo wa mifuko 100 ambapo 50 itaenda halmashauri ya Arusha na 50 halmshauri ya Meru ili ikakamilishe ujenzi wa madarasa kwenye maeneo mbalimbali yaliyobaki.
Mkoa wa Arusha ulikuwa na uwitaji wa madarasa zaidi ya 100 kwa ufaulu wa wanafunzi zaidi ya 20,000 na waliokuwa wamekosa nafasi ya shuleni zaidi ya elfu 17 kwa mkoa mzima hivyo ikapelekea juhudu za lazima kufanyika ili kujenga madarasa hayo na mpaka sasa ujenzi unaendelea maeneo mbalimbali.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa