Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameyakaribisha mashirika na Asasi za kiraia zinazofanya kazi mkoani Arusha, kuweza kushirikiana kwa karibu na ofisi yake na ofisi nyingine za Umma zilizopo kwenye maeneo yao, ili kuweza kushirikiana na kuongeza kasi katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mhe. Makonda ametoabrai hiyo wakati akifungua mkutano wake na wadau wa Mashirika na Asasi za kiraia, zinazoshughulika na maendeleo na huduma jamii, kwenye ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Gran Melia, mapema leo Julai 08, 2024.
Mhe. Makonda amezitaka Asas hizo kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kutatua changamoto za jamii kwa kuwa na uelewe wa pamoja katika kuyafikia malengo ya Serikali kwa kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Asas za kiraia kwa kufanya kazi pamoja itawarahisishia wananchi kupata huduma.
"Niwakaribishe kuitumia ofisi ya Mkoa na iwe kama sehemu ya ofisi yenu kwa jambo lolote na yeyote mwenye shughuli ndani ya mkoa wa Arusha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya mkuu wa wilaya ni ofisi yako, hivyo unapaswa kwenda kifua mbele na kuomba mahitaji yako ili ufanikishe kile unachokifanya ambacho sisi tunaamini ndicho kinachoweza kuleta tija kwenye maisha ya wananchi tunaowaongoza." ameongeza Mhe. Makonda.
Katika Mkutano huo wadau wa asasi hizo za kijamii zinazofikia takribani 1224, wanatoa maoni na changamoto zao kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ambaye ameahidi kuzifanyia kazi katika shabaha ya kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji wao wa kazi na kuweka mazingira rafiki ya mashirika hayo katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa