Na Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella amewaagiza Maafisa Elimu kata na Maafisa Watendaji wa kata, Mitaa na Vijiji kushirikiana na viongozi wa vijiji na mitaa katika maeneo yao, kuwatambua wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
Mhe. Mongella ameyasema hayo, alipotembelea na kukagua shughuli za maendeleo shule ya Sekodnari Madira kata ya Seela Sing'isi halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru, leo tarehe 29 Januari, 2024 na kupewa taarifa ya kuwa, bado kuna wanafunzi hawajaripoti shuleni ilihali wengine tayari wamekwisha kuanza masomo kuanzia tarehe 08 Januari, 2024.
Mhe. Mongella amewaagiza viongozi hao, kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa walioadikishwa kuanza darasa la awali na la kwanza pamoja na wale waliopangiwa kidato cha kwanza na hawajaripo shule,
ili kufahamu wanafunzi hao wako wapi.
"Wanafunzi wote wapo chini ya Mamalaka ya maeneo yenu, mkishirkiana na wenyeviti wa mitaa na vijiji watajulikana walipo, kwa wale wa kidato cha kwanza tumieni namba na majina yao pamoja na shule walizotokea kufahamu idadi ya waliohama, waliokwenda shule za binafsi na taarifa hiyo iwasilihswe ili kufanyia kazi wanafunzi ambao hawapo kokote" Amesisitiza Mhe. Mongella
Aidha, ameendelea kuwakumbusha wazazi kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto shule kwa kuwa hiyo ni haki ya mtoto kisheria na sio hiati, hivyo kwa mzazi ambaye atajulikana hajampeleka mtoto wake shule, hatua za kisheria zitachukuliwa juu yake na kusisistiza kuwa kila mtoto ana haki ya kwenda shule ikiwa ni Sheria na Sera ya serikali
Hata hivyo amewataka wakuu wa shule zote mpya zilizojengwa kusimamia upandaji wa miti, kuzunguka maeneo ya shule hizo, na kumkabidhi kila mwanafunzi mti wake wa kuutunza mpaka atakapohitimu masomo yake, lengo likiwa ni kuhifadhi na kutunza uasili wa mazingira hayo, ambayo yamehariniwa kwa kuwekwa majengo.
"Suala la utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti n8 jukumu la kila mwananfunzi, ikiwa ni sehemu pia ya masomo yake, walimu mkisismamia vema, tutaondokana na ukame lakini zaidi tutarithisha watoto hawa, tabia ya kupenda miti na kutunza mazingira yao kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo, hili liko ndani ya uwezo wenu walimu"Amebainisha Rc
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa