Na Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Jengo la wagonjwa wa Nje OPD Complex hospitali ya Jiji la Arusha mradi unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Mradi huo ni unatekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu shilingi bilioni 1 ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani wakati alipozindua hospitali hiyo mwaka 2021 na kutoa ahadi ambayo tayari serikali imezitoa na milioni 655 fedha za mapato ya ndani ya Jiji.
Hata hivyo Mhe. Mongella ameshukuru mheshimia Rais mama Samia kwa kuwajali na kuwathamini wananchi wa Arusha kwa kuwa hospitali hiyo ni muhimu kwa utoaji na upatikanaji wa huduma za afya na kuongeza kuwa licha ya kuwahudumia wananchi wa Jiji la Arusha lakini ni mkakati wa kupunguza msongamao wa wagonjwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Aidha amesema kuwa serilikali chini ya usimamizi wa mheshimiwa Rais, ameshatekeleza ahadi yake, kazi iliyobaki ni Jiji la Arusha kuendelea kutumia mapato yake ya ndani kukamilisha jengo hilo ili liweze kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 kuelekea 2025.
"Serikali katika kutekeeleza Ilani ya CCM mkoa wa Arusha, serikali imefanikiwa kujenga hospitali katika wilaya ya Karatu, Longido, Monduli na sasa inakamilisha hospitali hii ya wilaya ya Arusha pamoja na zahanati na vituo vya afya vya kutosha katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha" Ameweka wazi Mhe. Mongella
Amewataka watalamu wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha mradi huo, unakamilika kwa wakati ukiwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali.
Awali awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo wenye gharama ya Bilioni 1.6 utahusisha ujenzi wa sakafu ya chini ya jengo hilo, likibena ofisi za Idara ya dharura, idara ya mionzi, Idara ya ushauri wa kidaktari na usafishaji damu, pamoja na Huduma za uchunguzi wa mwili mzima.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa