Mkuu wa mkoa wa Arusha ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha leo tarehe 21 Desemba, 2023.
Mhe. Mongella amemuagiza mkuu wa shule hiyo, kuwasimamia walimu na wanafunzi, katika suala zima la utunzaji wa vifaa vya shule, ikiwemo majengo, kwa kuweka utaratibu wa utunzaji wa vifaa na majengo ya shule, ili yaweze kudumu kwa miaka mingi na kutumika kwa vizazi vijavyo.
Wakati huo huo, amewasisitiza walimu na kamati za shule, pindi fedha za ujenzi wa madarasa zinapokuja kwenye madarasa mawili iongezwe ofisi ya walimu, hata kama haiopo kwenye michoro ya ramani, jambo ambalo litapunguza gharama nyingine za ujenzi wa ofisi lakini zaidi litawezesha walimu kuwa karibu na wanafunzi na kurahisisha usimamizi.
"Tumeshakubaliana katika mkoa wa Arusha, tukipata za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, tuweke ofisi ya walimu katikatim kwa fedha hizo hizo, hii inawezekana na imeshafanyika halmashauri zote za mkoa, na haya ndio makubaliano yetu kama mkoa" Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule hiyo Mwl. Mwasisiti Kinyau, amebainisha kuwa, mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 679.1, ukiwa umejumuisha ujenzi wa vyumba 15 vya madarasa, ambweni mwawili na matundu 21 ya vyoo, unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni Barrik Gold Tanzania.
#arushafursalukuki
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa