"Sitaki kusikia kuna Migogoro na walimu, unyanyasaji au kuchelewesha malipo ya walimu katika Mkoa huu."
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akizindua miongozo ya uboreshaji wa elimu kwa Mkoa wa Arusha.
Sekta ya elimu ndio sekta mama katika sekta zote kwani ndiko kunazalishwa wataalamu mbalimbali.
"Itakuwa aibu sana ikiwa kama tunamiongozo hii alafu bado sekta ya elimu ikasua sua".
Amewataka maafisa elimu Mkoa na Halmashauri kufuata muongozo huo katika uteuzi wa wakuu wa shule ili kuondoa hali ya upendeleo na kuteuwa watu wasio na sifa ambao watazidi kuhariu sekta hiyo.
Amewasisitiza zaidi walimu kusimamia maadili ya wanafunzi huku wakishirikiana na wazazi ili kuondoka vitendo vya unyanyasaji kwa watoto.
Kupitia miongozo hiyo itaongeza molali ya kazi kwa walimu ambao wengi walionekana kukata tamaa ya kazi kutokana na changamoto mbalimbali walizokuwa wakipitia.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha bwana Missaile Musa amesema miongozo hiyo imegawanyika katika makundi 3, muongozo wa uteuzi wa viongozi kwa mamlaka za serikali za mitaa.
Vile vile kuna Muongozo wa kutatua changamoto katika sekta ya elimu na muongozo wa mkakati wa kuimarisha ufundishaji ngazi ya msingi.
Amesema kupitia miongozo hiyo mitatu sekta ya elimu itaimarika zaidi na kuwezo kuongeza kiwango cha ufaulu.
Nae Katibu Tawala Msaidizi Elimu bwana Abel Ntupwa amesema miongozo hiyo ilizinduliwa rasmi kitaifa na Waziri Mkuu Mkoani Tabora na kuitaka Mikoa yote izundue.
Hafla ya uzinduzi wa miongozo ya uboreshaji wa elimu Mkoani Arusha kilijumuisha Maafisa elimu kata hadi Mkoa, wakuu wa shule baadhi ya wanafunzi wa Msingi na Sekondari na wadau wa elimu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa