• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

VIONGOZI WA WANANCHI MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUSIMAMIA KWA KARIBU MIRADI KWENYE MAENEO YAO

Posted on: January 30th, 2024


Na Elinipa Lupembe


Viongozi wawakilishi wa wananchi wakiwemo wenyeviti wa vitongoji, vijiji, mitaa na kata, wamesisitizwa kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao, ili  kuhakikisha fedha zilinazotolewa  na Serikali zinatumika kulingana na malengo pamoja na kuilinda, kulinda na kuithamini miradi hiyo.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, alipotembelea na kukagua hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma kwenye Kituo cha Afya Mareu, Kata ya King'ori Wilaya ya Arumeru, na kukerwa na ucheleweshwaji wa matumizi ya fedha Sh. milioni 150, zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, kwenye kituo hicho.


Mhe. Mongella amewasisitiza viongozi wote na wananchi kushirikia katika hatua zote za utekelezaji wa miradi kwenye maeneo yao, kufuatilia hali ya ucheleweshwaji wa miradi ili kukamilika kwa wakati huku Serikali ilihali imetoa fedha za kukamilisha mradi husika.


Amewataka viongozi hao, kufanya ufuatiliaji wa mapokezi ya fedha katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kufahamu kiasi halisi cha fedha kilichotolewa na Serikali muda sambamba na utekelezaji wa mradi hadi kukamilika pamja na thamani ya mradi mzima.


"Nyinyi Wenyeviti wa vijiji, Madiwani na Wabunge fuatilieni matumizi ya fedha za miradi katika maeneo yenu, msiwaachie watalamu peke yao kwa kuwa miradi hii ni yenu, jukumu la kuisimamia ni lenu kama viongozi" Amesisitiza Mhe. Mongella.


Hata hivyo, Mhe. Mongella, amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, kufuatilia Sh.milioni 150, na kuhakikisha dawa na vifaa tiba zinanunuliwa kama ilivyokuwa maelekezo ya Serikali.


Pia alisisitiza kuwa samani zote za kituo hicho ziwe zimepatikana ikiwemo vitanda vya wagonjwa, samani za ofisi, Jenereta pamoja na kukamilisha ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji.


Naye Diwani wa Kata ya King'ori Mhe. Lucas Kaaya, licha ya changamoto hizo, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa kuwapa fedha nyingi za kutekeleza miradi katika kata hiyo, ikiwamo miradi ya afya, elimu, majina miundombinu na barabara miradi ambayo imeamsha ari ya maendeleo katika kata hiyo tofauti na awamu zilizotangulia.


Aidha alisema kuwa, wakati wa utekelezaji wa mradi huo, hakukuwa na maelewano mazuri baina ya viongozi na watalamu lakini kwa sasa wameshawekana sawa  mambo yameanza kwenda vizuri huku akiahidi kushirikiana na watalamu kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa.


Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kijiji Oldonyong'iru, Mhe. Timoth Paul Lihuni, amesema kuwa, tangu uongozi wa kituo hicho kubadilishwa kwa sasa, wananchi wameanza kufurahia huduma katika kituo hicho ikiwemo huduma ya upasuaji huku akiweka wazi kuwa hapo awali hawakushirikishwa.




Kituo hicho cha afya kimejengwa na serikali kwa gharama ya shilingi milioni 500  pamoja na milioni 150 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa