Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba serikali kuangalia zaidi utitiri wa sheria za kodi zinazowakandamiza ikiwemo ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wanaolipa kodi serikalini
Wakitoa maoni yao mbele ha Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue wafanyabiashara hao Pamoja na wadau mbalimbali wamesisitiza uthamini wa biashara za watanzania hata kama ni mdogo
Wafanyabiashara hao akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Kodi Tanzania Kanda ya Kaskazini, Nicholas Duhia na wengine akiwemo Adolf Locken ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wa Abiria Moose wa Arusha (AKIBOA ) wamesema wao kama chama waliwasilisha maoni yao kwa tume hiyo lakini kubwa zaidi ni kuhusu sheria za Kodi inayotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini pia kodi ya huduma ishuke kutoka asilimia 3 hadi kufika 0.1 kulingana na huduma walizotoa.
"Kila halmshauri ina malipo yake katika ulipaji wa ushuru wa huduma hii ni kero lakini wamiliki wa hoteli wameongezewa kodi ya huduma ya takataka wakati magari ya kuzoa taka ni machache hivyo kodi hizi ziwekwe katika dirisha moja ili walipaji walipe kodi kwa kiwango kidogo na si kodi kubwa zaidi huku mhusika wa biashara husika hanufaiki na biashara yake"
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi,Balozi Ombeni Sefue amewasihi wafanyabiashara hao kutoa mawazo yao ili kumsaidia Rais Dkt. Samia Hassan Suluhu kuja na mpango mzuri wa ukusanyaji wa kodi nchini na kuleta nafuu kwa wafanyabiashara hao
"Hakuna mtu yoyote atakayesumbuliwa wakati wa utoaji maoni juu ya ukusanyaji wa mapato hayo lakini Tanzania bado tupo nyuma katika ukusanyaji wa mapato tupo kwenye asilimia 12 lakini sasa tunahitaji kukusanyaji zaidi ya asilimia 15-16 ya mapato kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania "
Hata hivyo, Balozi Sefue aamemwagiza Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Viwanda, Biashara na Uwekezaji Sektretarieti ya Mkoa Arusha, Frank Mmbando kuhakikisha hakuna mtu yoyote atakayesumbuliwa katika utoaji wa maoni hayo kwani tume hiyo imeundwa na Rais Samia Hassan Suluhu kwaajili ya utatuzi wa kero za kodi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa