• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAAGIZWA KUSIMAMIA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Posted on: September 18th, 2024


OR-TAMISEMI ARUSHA



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata fursa ya elimu.



Akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi  Patandi Jijini Arusha Mhe. Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kufuatlia wazazi wanaowaficha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu kama stahiki ya mtoto wa Kitanzania.



“Nawaelekeza Viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia zoezi la ubainishaji na utambuzi wa awali wa watoto kwa wakati ili kubaini wenye mahitaji maalumu, kuwahimiza na kuhakikisha wazazi na walezi wanawapeleka watoto wao katika shule zilizoshauriwa na wataalamu ili wakaandikishwe na kuanza masomo na taarifa ya utekelezaji wake itolewe” amesema  Mhe. Mchengerwa.



 Mchengerwa amesema hadi kufikia mwaka 2020 kulikuwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu 28,482 lakini idadi hiyo imeongezeka mpaka wanafunzi 78,429 mwaka 2024 na Serikali imetenga jumla ya shule 6,088 zinazopokea wanafunzi hao na kuwapatia afua stahiki ambapo shule takriban 309 zina mabweni kwa ajili ya wanafunzi hao.



Naye Dkt. Magreth Matonya, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maalumu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia amesema malengo ya maadhimisho hayo ni kutangaza fursa za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinazotolewa na Serikali, kutangaza mafanikio yaliyopatikana, kutoa elimu ya uhamasishaji na pia kufanya tathmini ya elimu jumuishi. 



Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Maafisa Elimu wa Mikoa, Maafisa Elimu Watu Wazima Mikoa yote, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maafisa Elimu Maalum wa Halmashauri na Wadau mbalimbali wanaoihunga mkono Serikali.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa