Viongozi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha usafiri wa Treni unafiki katika Mkoa wa Arusha kwa usalama.
Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Kimanta, alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa tawala,Maafisa Tarafa na wenyeviti wa halmashauri ya jiji la Arusha na wilaya ya Arumeru.
Amesema maono ya Rais ni kuhakikisha treni inafika Arusha mwishoni mwa mwezi Agosti ili isaidie sekta ya usafirishaji na kuokoa muda wa wananchi kusafiri muda mrefu.
Ni miaka 30 imepita tangu treni ifike Mkoani Arusha,hivyo wananchi tunatakiwa kufurai na kuipokea kwa moyo mkunjufu.
Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa ajali kutoka shirika la Reli Tanzania bwana Maizo Mgedzi amesema, wananchi wanatakiwa kuchukua taadhari hasa kipindi ambacho treni itaanza kufanya kazi hasa wanaofanya shughuli mbalimbali karibu na reli.
Amesema ni hatari sana kufanya shughuli mbalimbali za kibinadamu karibu na reli kama kulima, kupitisha Wanyama,kuegesha Pikipiki na Magari,kuwa na Viwanja au kujenga karibu na reli.
Treni inaenda kuwa msaada mkubwa sana kwani itakuwa inaleta marighafi mbalimbali kwa ajili ya viwanda vilivyopo Arusha na hata kwa wafanyabiashara.
Mkoa wa Arusha kwa mara nyingine tena inaenda kuanzisha safari zake za Treni kutoka Mkoa wa Dar es Salaama hadi Arusha baada ya usafiri huo kusimama takribani miaka 30 sasa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa