Serikali kupitia RUWASA Mkoa wa Arusha katika kipindi cha bajeti 2021/2022 imeendelea kujenga miradi mipya,kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji maji vijijini, ambapo jumla ya miradi 66 yenye thamani Tsh.32,610,648,952.64 inaendelea kutekelezwa na ipo hatua mbalimbali za utekelezaji, Aidha, miradi hii ikikamilika itapunguza idadi ya vijiji visivyo na huduma ya maji rasmi kutoka 86 hadi 63, na hivyo kuboresha hali ya huduma ya maji vijijini kwa kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 70.2 ya sasa hadi asilimia 76.2, ifikapo Juni, 2022.
Katika bajeti ya 2021/2022 RUWASA Mkoa wa Arusha iliidhinishiwa jumla ya Tsh.10,276,348,023 Kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini, hadi sasa jumla ya Tsh.4,396,637,286.90 zimepokelewa sawa na asilimia 42.9 ya bajeti. Aidha, tulipokea bajeti ya ziada kiasi cha jumla ya Tsh. 2,470,881,598.03 kupitia program ya mpango wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji 5 vijijini ambapo hadi sasa utekelezaji unaendelea katika hatua mbalimbali.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa