MAJUKUMU YA SEKSHENI YA HUDUMA YA URATIBU NA USIMAMIZI WA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA:
Kushauri na kusimamia matumizi bora ya rasilimali fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kukuza na Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza utawala bora;
Kuwezesha mapitio ya muundo na michakato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kushiriki katika kaguzi za kawaida/kushtukiza zinazohusu utendaji kazi na majukumu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuandaa bajeti na matumizi;
Kuratibu na kushauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala ya kiutumishi (kuajiri, kujaza nafasi wazi, masuala ya kinidhamu, kupandisha madaraja n.k);
Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na masuala yoyote kiutumishi;
Kuratibu, kuandaa, kutekeleza, usimamizi na ufuatiliaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusiana na mkataba wa huduma kwa mteja;
Kumshauri Katibu Tawala Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa sheria za kazi.
Ukusanyaji Mapato ya Ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hali ya ukusanyaji wa Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa umeendelea kuimarika. Kwa mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri za Mkoa wa Arusha zilikadiria kukusanya jumla ya shilingi 42,381,671,000 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani na Mapato. Aidha, Kwa kipindi cha Julai hadi Machi, 2022 Halmashauri za Mkoa wa Arusha zilikusanya jumla ya shilingi 30,795,617,786 sawa na asilimia 73 ya makadirio yaliyoidhinishwa kwa kila Halmashauri kama ifuatavyo:
Na. |
Halmashauri |
Makisio ya mwaka 2021/22 |
Mapato hadi Machi, 2022 |
Asilimia |
1 |
Arusha CC
|
23,295,000,000 |
18,047,921,155 |
77 |
2 |
Monduli DC
|
2,250,000,000 |
1,661,833,415 |
74 |
3 |
Ngorongoro DC
|
2,753,000,000 |
1,420,425,065 |
52 |
4 |
Karatu DC
|
3,964,000,000 |
3,082,619,229 |
78 |
5 |
Meru DC
|
3,499,000,000 |
2,655,103,478 |
76 |
6 |
Arusha DC
|
4,383,000,000 |
2,699,865,822 |
62 |
7 |
Longido DC
|
2,239,000,000 |
1,227,849,622 |
55 |
|
Jumla ndogo
|
42,383,000,000 |
30,795,617,786 |
73 |
Halmashauri zimetoa jumla ya shilingi bilioni 8.9 ikiwa ni asilima 40/60 ili kugharamia miradi ya maendeleo sawa na asilimia 52 ya Mapato ya Ndani hadi kuishia Machi, 2022.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa