Utekelezaji wa Miradi ya Elimu kupitia Fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Mkoa wa Arusha umekuwa ukipokea fedha za utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi na ukamilishaji wa miundo mbinu mbalimbali katika Shule za msingi na Sekondari, miradi hii imeboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia walimu. Miradi hii ni Ujenzi wa Madarasa, Mabweni, Matundu ya vyoo, Nyumba za Walimu, Maabara, Mabwalo, Ofisi za Walimu na Maktaba.
Katika kipindi cha mwezi Julai 2021- Februari 2022, Halmashauri za Mkoa wa Arusha zimetenga jumla ya shilingi milioni 884.15 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu 158 katika Shule za Msingi. Hadi kufikia mwezi Machi, 2022, miundombinu 83 ilikuwa hatua ya ukamilishaji na miundombinu 75 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Kwa upande wa Elimu Sekondari, kwa kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Februari, 2022, Mkoa umetenga jumla ya shilingi bilioni 1.088 kwa ajili ya ujenzi wa jumla ya miundombinu 192 ya mabweni, vyumba vya madarasa, nyumba za watumishi, matundu ya vyoo, Maabara na majengo ya utawala katika Shule za Sekondari. Aidha, hadi kufikia Machi, 2022, jumla ya miundombinu 116 ipo hatua ya ukamilishaji na miundombinu 78 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaj
Mkoa wa Arusha ulipokea jumla ya shilingi bilioni 1.92 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 96 ya Shule Shikizi kutoka fedha za UVIKO-19. Hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya madarasa 92 yalikuwa yamekamilika sawa na asilimia 95 ya madarasa yote shikizi. Aidha, fedha za madarasa 4 ya Shule Shikizi ya Wilaya ya Ngorongoro katika Tarafa ya Ngorongoro zimeshahamishiwa Wilaya ya Handeni.Ujenzi wa Madarasa ya Shule za Sekondari kupitia Fedha za UVIKO-19
Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya shilingi bilioni 8.34 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 417 ya shule za sekondari. Hadi kufikia Machi, 2022, jumla ya madarasa 386 yalikuwa yamekamilika kwa asilimia 100 ikiwemo utengenezaji wa viti 50 na meza 50 kwa kila darasa. hii ni sawa na utekelezaji wa asilimia 93 ya madarasa yote. Madarasa 31 ya ghorofa kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha (19) na Wilaya ya Arusha (12) yako katika hatua ya ukamilishaji kama kupaka rangi. Aidha, madarasa 12 ya Tarafa ya Ngorongoro katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro yalikuwa hayajaanza ujenzi kutokana na kutopata kibali cha ujenzi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na fedha zake zimehamishiwa katika Halmashauri ya Handeni.
Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya shilingi milioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili kwa Shule za Msingi zenye Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum kwa Wilaya za Ngorongoro na Meru. Bweni la Wilaya ya Meru lipo katika hatua ya upauzi na bweni la Wilaya ya Ngorongoro ambalo lipo kwenye Tarafa ya Ngorongoro halijaanza kujengwa kutokana na kukosa kibali kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngoron
Halmashauri za Arusha,
Arusha Jiji na Monduli zilipokea jumla ya shilingi milioni 860.5 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu 70. Hadi Machi 2022 jumla ya shilingi milioni 483.76 zilikuwa zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo. Miundombinu hiyo ambayo ni madarasa, matundu ya vyoo na mifumo ya uvunaji maji ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na kazi zinaendelea.
Ukamilishaji wa Vyumba vya Madarasa ya Sekondari kwa Fedha za TOZO
Mkoa wa Arusha kutokana na fedha za Tozo ulipokea jumla ya shilingi milioni 162,500,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 13 ya Shule za Sekondari ambapo kila darasa lilipokea shilingi 12,500,000. Fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya kumalizia vyumba vya madarasa vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi miradi hiyo imekamilika.
Mkoa wa Arusha ulipokea kiasi cha shilingi milioni 508.62 fedha kutoka Vyanzo vya Nje (Foreign) kwa ajili ya utekelezaji wa jumla ya miundombinu 343 katika shule za Msingi na Sekondari ambapo kati ya miundombinu hiyo, vyumba vya madarasa ni 17, madawati 220, Hosteli 1, Nyumba ya Mwalimu 1 na matundu ya vyoo ni 102. Lengo ni kuboresha miundombinu na mazingira ya kujifunzia. Utekelezaji umefanyika katika Halmashauri za Arusha, Monduli na Ngorongoro na utekelezaji upo katika hatua za ukamilishaji.
Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya shilingi bilioni 4.7 kwa ajili ya ujenzi wa Shule za Sekondari mpya kumi (10) katika kata 10 zisizokuwa na Shule za Sekondari kupitia Program ya Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP). Ujenzi wa shule hizi upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Ujenzi wa Vyumba vya Maabara katika shule za Sekondari
Kuhusu miundombinu ya shule za Sekondari, hususani ujenzi wa maabara za sayansi, Mkoa wa Arusha mwaka 2020 ulikuwa na vyumba vya maabara za 326 hata hivyo kufikia Machi, 2022 Mkoa umefanikiwa kujenga maabara 401 kwa mchanganuo zikiwemo ufuatao biolojia, 130 kemia 137, fizikia112 na Tehama 22.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa