Utangulizi
Kuhusu Vituo vya Kutolea huduma ya Afya, Serikali ya Mkoa iliendelea kuweka msisitizo katika upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia jumla ya vituo 408 vinavyotoa huduma za Afya, zikiwemo hospitali 19, vituo vya afya 61 na zahanati 328. Mkoa umeweka jitihada za dhati katika kuongeza idadi kwa idadi ya vituo vya kutolea huduma za Afya kutoka vituo 392 mwaka 2020 hadi vituo 408 mwaka 2021 hadi Machi, 2022. Kati ya vituo 408 vya kutolea huduma vilivyopo, Serikali inamiliki vituo 234 (57%), taasisi za umma 15 (4%), watu na taasisi binafsi vituo 159 (39%).
Miradi ya Afya kupitia Mapato ya Ndani.
Katika kuhakikisha kuwa huduma za Afya kwa wananchi zinaboreshwa, Serikali ilibuni na kutekeleza mradi wa ujenzi na ukamilishaji miundombinu ya afya katika Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha, kwa gharama ya Shilingi bilioni 3.8 zilitolewa kupitia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri na hadi kufikia mwezi Machi,2022 shilingi bilioni 1.32 zimetumika sawa na asilimia 34.8. Vituo hivi viko katika hatua mbalimbali za ujenzi. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya vipya, Zananati, kuchangia ujenzi wa Hospitali za Wilaya na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya afya katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Miradi ya Afya kupitia Fedha za Ruzuku ya Serikali Kuu.
Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha Julai hadi Feb, 2022 umepokea fedha za ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya afya jumla ya shilingi bilioni 2.5. Miradi ya afya inayohusika ni pomoja na ukamilishaji wa vituo vya Afya, ukamilishaji wa nyumba za watumishi wa afya, ujenzi na ukarabati wa Zahanati pamoja na ujenzi wa Hospitali za Wilaya ikijumuisha Hospitali ya Jiji la Arusha.
Miradi ya Afya kupitia Fedha za Tozo.
Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha Julai hadi Februari,2022 ulipokea fedha za TOZO jumla ya shilingi bilioni 1.75 ikiwa ni sawa na shilingi milioni 250 kwa kila Halmashauri za Mkoa wa Arusha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya kwa tarafa zisizokuwa na Vituo vya Afya. Hadi Machi,2022 jumla ya shilingi bilioni 1.34 zilikuwa zimetumika kwa ajili ya ujenzi na hatua zilizofikiwa ni kama zinavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali Na.9: Mchanganuo wa Vituo vya Afya vinavyojengwa kwa Fedha za TOZO
Halmashauri
|
Kata
|
Jina la
Mradi |
Kiasi cha fedha kilichopokelewa |
Kiasi cha fedha kilichotumika |
Hatua ya utekelezaji |
Arusha Jiji
|
Terrat
|
Kituo cha Afya Mkonoo
|
250,000,000.00 |
121,000,000.00 |
Upauzi
|
Arusha DC
|
Mwandeti
|
Kituo cha Afya Engalawon
|
250,000,000.00 |
152,060,678.00 |
Umaliziaji
|
Meru DC
|
King’ori
|
Kituo cha Afya Mareu
|
250,000,000.00 |
164,678,900.00 |
Umaliziaji
|
Longido DC
|
Ketumbeine
|
Kituo cha Afya Ketumbeine
|
250,000,000.00 |
237,000,000.00 |
Umaliziaji
|
Karatu DC
|
Baray
|
Kituo cha Afya Mbuga Nyekundu
|
250,000,000.00 |
219,000,000.00 |
Umaliziaji
|
Monduli DC
|
Kisongo
|
Kituo cha Afya NAFCO
|
250,000,000.00 |
240,453,438.00 |
Umaliziaji
|
Ngorongoro DC
|
Sale
|
Kituo cha Afya Sale
|
250,000,000.00 |
215,378,265.00 |
Umaliziaji
|
Jumla |
1,750,000,000.00 |
1,349,571,281.00 |
|
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Machi 2022
Mkoa wa Arusha kwa kipindi cha Julai hadi Machi,2022 ulipokea fedha za UVIKO-19 jumla ya shilingi bilioni 1.99 kwa ajili ya ujenzi wa Majengo ya Huduma za Dharura (EMD) kwa Halmashauri za Arusha Jiji, Meru, Ngorongoro na Karatu, ikiwa ni mgao wa shilingi milioni 300 kwa kila Halmashauri 3, Pamoja na Tshi Milioni 540 kwa kila Halmashuri shilingi milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi idara ya afya kwa Halmashauri za Wilaya zote isipokuwa Jiji la Arusha. Miradi yote ilianzwa kutekelezwa mwezi Machi, 2022 ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji.
Aidha, Wilaya ya Longido imepokea kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Huduma za Wagonjwa Mahututi (ICU) ambao upo hatua ya awali ya ujenzi.
Uboreshaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mt Meru
Juhudi za Serikali za kuboresha huduma za afya katika Hospitali i ya Rufaa ya Mkoa, Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru imepokea jumla ya shillingi Bilioni 3.97 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa ambavyo havijawahi kuwepo katika hospitali hii tangu kuanzishwa kwake. Vifaa hivyo ni: -Vifaa vya Dharura shilingi milioni 771, Vifaa vya Huduma za wagonjwa Mahututi Shilingi milioni 660, CT Scan Shilingi Bilioni 2.3 na Digital X-ray Shilingi milioni 240.
Aidha, miradi yote hiyo inaendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali na itakapokamilika itaboresha huduma kwa wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali ya Rufaa na hivyo itapunguza rufaa ya baadhi ya magonjwa zinazopelekwa Hospitali za Muhimbili na KCMC.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa