Serikali yahimiza matumizi yaTeknolojia ya uhifadhiwa nyaraka huku asilimia 53 ya taasisi za Umma zikiwa tayari zikitumia mfumo wa ofisi mitandao (e-office) katika utunzaji wa kumbukumbu, ikiwemo uhifadhi na usimamizi wa nyaraka kidigitali na kuleta ufanisi zaidi katika utendaji wa kazi nchi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, Xavier Daud wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 59 Bodi ya Baraza la Wahifadhi Nyaraka Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESARBICA), mapema leo Agosti 19, 2024 mkoani Arusha.
Amesema kuwa, nchi ya Tanzania imesonga mbele katika matumizi ya mfumo wa kidijitali kwenye ofisi za Umma, mfumo ambao umerahisisha utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali, mfumo ambao licha ya urahisi wa utoaji na upatikanaji wa huduma kwawananchi, umetoa fursa ya kupokea maoni na malalamiko kutoka kwawananchi na kutoa mrejesho.
"Tanzania kwa sasa tumesonga mbele katika mfumo wa kidigitali kwakutumia mfumo wa e-office unaorahisisha wananchi kupata huduma katika taasisi za Umma, usimamizi na uhifadhi wa kumbukumbu za kidijitali pia mfumo wa e-mrejesho unasaidia kukusanya maoni na malalamiko ya wananchi kidigitali"
Naye Rais wa ESARBICA, Puleng Kekana amewataka wanachama wa nchi hizo kuchukua hatua za kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo kwa taaluma za kumbukumbu haswa vijana, wanaharakati ili kuhakikisha utoaji huduma bora kwa wananchi ikiwemo jamii Kuweza kutunza kumbukumbu vizuri.
Mkutano huo wa siku mbili wenye lengo la kubadilishana uzoefu wa nchi wananchama kuhakikisha sekta hiyo ya utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka katika Serikali ya nchi hizo inaboreshwa na kuhakukisha zinatunzwa na kuhifadhiwa vizuri ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa