Kamishina wa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Sivangilwa Mwangesi, amesema viongozi wakiwa waadilifu itawapa wananchi imani na Serikali yao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha maadili kwa viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, Halmashauri na taasisi za Serikali za Mkoa wa Arusha, Katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Tukiwajengea wananchi imani na Serikali yao itawarahisishia utendaji wao wa kazi wa kila siku katika kujipatia vipato".
Maadili ya Viongozi yanaongozwa na Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella ameiyomba Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma kuendelea kutoa elimu zaidi kwa Jamii.
Kwani Jamii inafahamu kiongozi akiitwa na sekretarieti ya maadili anakuwa ni mtovu wa nidhani na anastahili kuadhibiwa.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amesema watumishi wa Umma wanatakiwa kutunza siri za mahali pa kazi hasa za wateja wanaowahudumia.
Ameiyomba Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma kutunga Sheria itakayowawajibisha watumishi wa Umma ambao watatoa siri za ofisi.
Kamishina wa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Sivangilwa Mwangesi amefanya ziara ya siku moja katika Mkoa wa Arusha na kuwakumbusha Viongozi wa Mkoa umuhimu wa kuzingatia maadili ya kazi kwa watumishi wa umma.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa