Mkoa wa Arusha umebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali kulingana na hali ya kijiolojia. Kati aina ya miamba hiyo saba (7) aina nne za miamba zinapatikana katika mkoa wa Arusha.
Kuna ukanda wa Mozambique belt ambao ni maarufu kwa madini ya vito kama vile Ruby, anyolite, corundum, Rhodolite, Green Garnets, Red garnets, sperssartite,Tourmaline, Emeralds, sunstones, moonstones, Aventurine Quartz, aquamarine na Kinywe na miamba chokaa n.k.
Kuna ukanda wenye miamba ya volcano na bonde la ufa ambako kuna ya Niobium (Rare Earth Elements) Apatite, zeolites, Florite, Bentonite, gesi ya Helium pozzolana (Madini ya Viwandani) na madini ujenzi.
Mkoa wetu wa Arusha wenye ukubwa wa Kilometa za mraba 37,576 una jumla ya
Pamoja na utalii, Vilelvile umekuwa ni kitovu cha biashara ya madini hasa ya vito. Madini hayo yanatoka ndani ya Mkoa au nje ya Mkoa kama vile, Manyara, Tanga, Morogoro, Lindi na Ruvuma. Pia hata nchi za nje kama Ethiopia, Mozambigue, Zambia na Congo.
Umaarufu huu wa mkoa wa Arusha umejengeka kwa Zaidi ya miaka 30 iliyopita. Kwa kipindi cha mwaka wa Serikali 2018/19, Ofisi ya Madini Arusha ilikuwa na:
Takwimu za biashara ya madini kwa Mkoa wa Arusha kwa mwaka 2018/19 (Yaani tangu July 2018 mpaka 30 June 2019) zinaonesha kuwa madini yenye thamani ya 21,074,505,883.43 TZS yaliuzwa na mrabaha uliopatikana ni 764,385,283.88 TZS na Ada ya ukaguzi 208,653,073.56 TZS.
Takwimu hizi zinaonesha kuwa mapato yanayokusanywa kutokana na biashara ya madini Mkoani Arusha ni asilimia 40% ya maduhuli yote katika sekta ya madini mkoani Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa