Ufugaji ni moja ya shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na inakadiriwa kuna jumla ya ng’ombe wa asili 1,670,770; ng’ombe wa maziwa 198,330; mbuzi 2,043,201 na kondoo 1,848,028 wanaochungwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 1,065,392.92 sawa na asilimia 31 ya eneo lote la Mkoa. Hali ya upatikanaji wa malisho ya mifugo hutofautiana kati ya maeneo na misimu kutegemeana na mtawanyiko wa mvua.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa