Serikali ya Awamu ya Sita imeweka bayana na kuifanya sekta ya viwanda kuwa mhimili wake mkuu wa kuiwezesha nchi yetu kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Hivyo, katika kutekeleza Ilani, Serikali imeweka msukumo mkubwa zaidi katika kuimarisha uzalishaji katika viwanda vilivyopo, kufufua na kujenga viwanda vipya.
Aidha, Sekta ya Viwanda na Biashara ina lenga kuendeleza na kuimarisha maendeleo endelevu ya viwanda katika kuchangia ukamilishaji wa dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. Katika kutekeleza dhima ya maendeleo endelevu ya viwanda na dira ya Taifa ya 2025.
Katika utekelezaji wa malengo hayo, Mkoa umefanikisha uazishwaji Viwanda vidogo 120 kwa mchanganuo ufuatao; Jiji la Arusha 26, Halmashauri za Wilaya za Arusha 14, Karatu 60, Meru 10, Monduli 5 na Ngorongoro 5 na Viwanda vikubwa 1 na kati ni 9. Aidha, jumla ya ajira mpya zaidi ya 709 zimezalishwa kutokana na viwanda vilivyoanzishwa. Maeneo ya Uwekezaji yaliyotengwa
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa