Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amezitaka halmshauri zote Mkoani hapo kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini ( TARURA) na Wakala wa barabara Tanzania(TANROAD) kumaliza barabara zote zinazojengwa kwa umbali wa Kilomita 1 kukamilika ifikapo Januari, 2023.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha 46 cha bodi ya barabara Mkoa wa Arusha.
"Hakuna haja ya kutumia muda mrefu kujenga barabara zenye kilomita 1 na kuwafanya wananchi kukosa huduma".
Miundombinu ya barabara ni kichocheo muhimu cha kujenga uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Amesema, serikali imeongeza bajeti ya barabara kwa kiasi kikubwa ili kurahisisha barabara kukamilika kwa wakati, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 TARURA wamepatiwa fedha kiasi cha bilioni 18.2 na kwa mwaka 2021/2022 bajeti ilikuwa bilioni 9.
Kwa upande wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) bajeti ya mwaka 2021/2022 ilikuwa Milioni 13 na kwa mwaka wa fedha 2022/2023 bajeti ni milioni 12.9 kwa mtandao wa barabara wa kilomita 1,493.12 kwa kiwango cha lami na changalawe.
Amewataka viongozi wa Wilaya na Halmshauri kwenda kusimamia na kufahamu mitandao ya barabara iliyopo katika maeneo yao.
Kikao cha bodi ya barabara Mkoa kimefanyika katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.