Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru, kata ya Usa River mapema leo Juni 4, 2024
Katika Mkutano huo, Dkt. Nchimbi ametumia wasaa huo kuzungumza na wanachi pamoja na kusikiliza kero, kero ambazo baadhi yake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amezitolea ufafanuzi na kuahidi kuendelea kutembelea wananchi kwenye maeneo yao ili kuwagikia na kutatua kero hizo.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo, amemtaka Mhe. Makonda kuendelea kufuatilia kero na matatizo ya wananchi kwenye maeneo yao ili kufikia malengo ya Serikali ya kuhudumia wannachi pamoja na kutatua kero zao.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi na Serikali yake ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutokana na kazi kubwa inayoifanywa ya kupelekea huduma za kisekta karibu na wananchi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.