Na Elinipa Lupembe
Serikali kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari - SEQUIP, imetua shule ya sekondari Mringa halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru na kutoa shilingi milioni 100 na kufanya ukarabati mkubwa wa mabweni manne.
Makamu mkuu wa shule sekondari Mringa Mwl. Kleruu Zakaria Sumaye, amesema kuwa, kiasi hicho cha fedha kimetumika kufanya ukarabati mkubwa wa mabweni manne shuleni hapo, mabweni ambayo yanauwezo wa kulaza wanafunzi 160, wanafunzi 40 kwa kila bweni.
Shule ya sekondari Mringa ina jumla ya wanafunzi 1,962, Wasichana 1,342 na wavulana 620 wa kidato cha kwanza mpaka cha sita, huku kidato cha tano na sita wakiishi bweni na kidata cha kwanza mpaka cha nne ni wanafunzi wa dahalia (hostel)
Ameyataja manufaa ya mabweni hayo pamoja na kupungumza msongamano wa wanafunzi kulala bweni moja, zaidi yatakuwa ni mazingira salama kwa wasichana wanaolala shuleni hapo kwa kuwa shule hiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi wasichana ukilinganisha na wavulana, ambao wamepewa kipaumbele kutokana na changamoto zinazowakumba wanaposoma shule za kutwa.
Mwl. Kleruu, ameongeza kuwa uwepo wa mabweni shuleni licha ya kuongeza ari ya wanafunzi kujisomea lakini pia inatoa fursa kwa walimu kuwasimamia wanafunzi muda wote, jambo ambalo wanategema litapandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu
Awali mabweni hayo chakavu yalijengwa tangu mwaka 1953 yakiwa na umri wa miaka 70 sasa
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.