Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi amepokea Mwenge wa Uhuru 2024 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Meru, Mwl. Zainabu Makwinya, kwenye Soko la Chekereni kata ya Kiserian,wilaya ya Arumeru leo Julai 20, 2024.
Ukiwa katika Halmashauri ya Arusha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava atakimbiza umbali wa Kilomita
145.3 na kukagua miradi 6 yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.09.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru utatembelea mradi wa Uhifadhi wa chanzo cha maji Mungusi kata ya Mlangarini, Kikundi cha Vijana Agri-genius Youth Group Mlangarini wenye thamani ya shilingi milioni 30, kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Mafuya cha Puma Oloirien, mradi wenye tahamni ya shilingi milioni 590, kutembelea Mradi wa Shule ya Enaboishu Academy wenye thamani Milioni 460.9
Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru utazindua Mradi wa Ujenzi wa Mabweni mwaili ya wasichana shule ya sekondari Mringa yaliyojengwa na Serikali kupitia mradi wa SEQUIP kwa gharama ya shilingi milioni 260, atatembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Habari Maalum - Hospitali ya Olturumet mradi wenye thamani ya shilingi milioni 474.9, ataweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Majengo manne (wagonjwa wa nje(opd), mionzi, maabara na mochwari)) hospitali ya Halmashauri ya Arusha Olturumet wenye thamani ya shilingi milioni 900, atatembelea Mradi wa Maji Safi Oldonyosambu wenye thamani ya shilingi bilioni 6.38 pamoja na kutembelea chuo cha ufundi Olkokola
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeee
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.