Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, akielezea umuhimu wa mkutano wa Halmashauri Kuu Iliyoboreshwa, unaofanyika mara baada ya Kamati ya Siasa kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye halmashauri za mkoa wa Arusha, leo Machi 21, 2024
Mwenyekiti Sabaya, ameweka wazi kuwa, Ofisi ya Chama mkoa wa Arusha, imeamua kuanzi Mkutano huo mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo kwa lengo la kupata taarifa za miradi yote ya halmashauri husika kutoka ngazi ya Kata.
Amesema kuwa, katika mkutano huo, Maafisa Watendaji wa Kata, watawasilisha shughuli zote zinazofanyika kwenye kata zao, ikiwemo utekelezaji wa miradi ya amendeleo kwenye kata zao.
"Baada ya Kamati kukagua Miradi ya maendeleo, tunahitaji kupata taarifa kutoka kwenye kata, kila Afisa Mtendaji afahamu mira kwenye eneo lake, gharama ya mradi, chanzo cha fedha na muda wa utekelezaji wa miradi yote, pamoja na kuwasilisha changamoto zinazokabili eneo husika" Amesema Sabaya
Mkutano huu, umefanyika kwenye hotel ya Ace Age, eneo la USA, umewakutanisha Kamati ya Siasa Mkoa, kamisaa wa Mkoa, Kamati ya Siasa Wilaya ya Kichama ya Meru na Kamisaa wa wilaya, Viongozi wa chama ngazi ya kata, Maafisa Watendaji wa kata pamoja na watalamu timu ya menejimenti halmasahuri ya Meru na Sekretariet ya mkoa wa Arusha.
Awali, Mkutano huo ndio hitimisho la ziara ya Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha ya kukague Utekelzaji wa Ilani ya CCM Mkoa kwa kipindi cha Julai - Decemba, 2023, ambapo imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwenye sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu ya Barabara, kwenye wilaya sita na halmashauri saba za mkoa wa Arusha ambazo ni Jiji la Arusha, Halmasahuri ya Arusha, Longido, Karatu,Meru Monduli na Ngorongoro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.