Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumapili Septemba 29, 2204 anashiriki Ibada maalum ya Kanisa la KKKT Usharika wa Kimandolu Jijini Arusha kwaajili ya kumstaafisha kwa Heshima Baba Askofu Dkt. Solomon Jacob Massangwa ambaye ni Askofu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Askofu Massangwa amekuwa Mchungaji tangu mwaka 1982 na kutumika katika usharika wa Arusha Mjini akiwa Mchungaji Mwenza wa Usharika na baadae Mchungaji Kiongozi kabla ya mwaka 1993 kuteuliwa kuwa Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.