WANANCHI WATAKIWA KUUNGANISHA NYUMBA ZAO NA MIFUMO YA MAJITAKA ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Arusha wanaojenga nyumba za kuishi na za biashara kuunganisha nyumba zao na mifumo ya Majitaka iliyopo Mkoani Arusha ili kuhakikisha wananchi hao wanatumia vyema mifumo iliyopo Jijini Arusha na kuondokana na matumizi ya Majitaka.
Kulingana na Mkuu huyo wa Mkoa, Arusha ndiyo wenye mradi mkubwa zaidi wa majitaka nchini Tanzania, akiwataka wote wanaotaka kujifunza kuhusu mifumo ya Majitaka kuja Mkoani Arusha kujifunza kuhusu utendaji wa mifumo hiyo ya Majitaka.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.