Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameondoka mkoani Arusha na kusindikizwa na Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkowa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali kwenye kiwanja cha Ndege Arusha Novemba 04, 2024.
Waziri mkuu ameondoka mkoani Arusha mara baada ya kushiriki Mikutano miwili ya Mtandao wa Mameneja na Wasimamizi wa Rasilimali Watu katika sekta za Umma Barani Afrika pamoja na Mkutano wa Afya ya Pamoja Iliyofanyika mkoani Arusha kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) tarehe 04, Novemba, 2024
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.