• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

DCEA YATOA MAFUNZO KWA ASAS ZINAZOHUDUMIA WARAHABU KANDA YA KASKAZINI

Posted on: January 14th, 2024

Na Daniel Gitaro

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa mafunzo kwa Asasi za kiraia zinazotoa huduma kwa waraibu wa Dawa za Kulevya juu ya uandishi mzuri wa maandiko ya miradi itakayowawezesha kudhibiti matumizi ya dawa hizo nchini.


Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Misaile Albano Mussa, Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Mali, Hargeney Chitukuro amesema kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwa Asasi hizo ili kutoa elimu zaidi na matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya sambamba na umakini wa matumizi ya fedha kwaaajili ya utekelezaji wa kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini.


Ameongeza kuwa, uandikaji wa maandiko ya miradi ni muhimu yakazingatiwa  ili kusaidia Serikali katika mapambano ya matumizi ya dawa hizo za kulevya sanjari na udhibiti wake kwa kuibua miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa Jamii kuanzia shuleni, vyuoni, Taasisi za fedha na n.k.


Naye Afisa Maendeleo ya Jamii ofisi ya DCEA Kanda ya Kaskazini, Sarah Ndaba amesema elimu hiyo ya uandishi wa maandiko ni muhimu kwani itasaidia wadau hao katika kusaidia Jamii kupata elimu pamoja na ufanyaji kazi kwa ufanisi zaidi na kuisaidia Serikali kwenye mapambano hayo.


Vileile amsema kuwa, mamlaka hiyo ina jumla ya Asasi zaidi ya 100 na kwa Kanda ya Kaskazini wanashirikiana na Asasi zaidi ya 16 ambazo zinatoa mrejesho juu ya udhibiti wa dawa hizo pamoja na utoaji mrejesho kwa mamlaka ya DCEA juu ya mchanganuo wa kazi walizofanya na watakazofanya kwa kila mwaka.


"Lazima kuwe na weledi katika uandishi wa maandiko yao ili kupata uelewa na mbinu mpya ya maandiko bora ya kushawishi wafadhili kutoa fedha kwaaajili ya mapambano hayo nchini kwani Asasi za kiraia zina umuhimu mkubwa wa kupambana na dawa hizo ikiwemo utoaji elimu kwa jamii". Amesema.


Naye mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Shirika la Gift of Hope Foundation ,la  Mkoani Tanga, Said Bandawe amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwani yatawasaidia kupata fedha sanjari na kufanya harambee ili kukusanya fedha kwaaajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kudhibiti dawa hizo ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii zote.


Wakati huo huo, Afisa Elimu wa Mamlaka hiyo (DCEA), Shabani Miraji ameongeza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kudhibiti dawa hizo sambamba na utoaji elimu zaidi na kubaini mbinu mpya  wanazotumia wafanyabiashara wa dawa hizo na jinsi ya kuwadhibiti.




Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa