• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC KIHONGOSI: ARUSHA IWE SEHEMU SALAMA YA UPENDO, AMANI NA MSHIKAMANO...

Posted on: July 1st, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenan Laban Kihongosi  amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano na sio kufanya kazi kwa mashindano, kwa kutambua wote wanajenga nyumba moja,  ili mmoja akiwa bora wote wawe bora na Arusha iwe salama ya upendo amani na mshikamano na kubainisha kuwa, hapendezwi kuona watu wakiharibikiwa kwenye maisha yao ya kazi.


Mhe. KIihongosi ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Gloriana Julius Kimath na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Mwinyi Ahmed Mwinyi, ikiwa ni jukumu lake la kwanza mara baada ya kukabidhiwa Ofisi,  Juni 30,2025.


Amesema kuwa, kila mtumishi anawajibu wa kuwatumikia wananchi kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa  kushirikiana na kusaidiana na wengine ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwaletea  wananchi  maendeleo na kuacha na tabia ya mashindano kwa wote wanatekeleza dhamana waliyopewa na kuaminia na Serikali.


"Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa bila kujali hali yake, kama viongozi tunao wajibu wa kuwahudumia watu kwa heshima kwa  kuzingatia Kanuni,  heria na taratibu za Utumishi wa Umma, tusipende kuonea watu, kwa kuwa kila mtu ana nafasi yake, tutambue kuwa tumekutanishwa kwenye kazi kwa kusudi ya Mungu, hivyo majungu na fitina hazina nafasi baina yetu".Amebainisha Mhe.Kihongosi.


Amesisitiza kuwa, katika kufanya kazi kwake, majungu na fitina viwe mwiko, kuwa hataweza kumhukumu mtu bila kufanya nae kazi, na kuongeza kuwa anatamani kuwafahamu  watu kwa uwajibikaji wao anapofanya nao kazi na sio kuambiwa maneno na mtu na mtu mwingine.


"Tusaidiane, tuhurumiane, tuheshimiane, tuambiane ukweli kwa nidhamu, kila mtu awe baraka kwa mwingine, tusifurahie wengine wakiharibikiwa, tuwe baraka kwa watu wote, kila mtu afanye kazi kwa kutambua thamani ya mwingine kwa kuwa tunajenga nyumba moja, tuweke mbali chukii huku kipaumbele chetu kikiwa ni kutatua migogoro na changamoto za wananchi wetu ili kazi iendelee.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC KIHONGOSI ATEMBELEA OFISI ZA CCM MKOA WA ARUSHA..

    July 02, 2025
  • RC KIHONGOSI AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI NA MILA; ASISITIZA KUOMBEA AMANI..

    July 02, 2025
  • RC KIHONGOSI: ARUSHA IWE SEHEMU SALAMA YA UPENDO, AMANI NA MSHIKAMANO...

    July 01, 2025
  • UAPISHO

    July 01, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa